Mazao yana mahitaji tofauti ya virutubisho ambayo huathiri usawa wa udongo katika hali tofauti. Mpango mzuri wa mzunguko wa mazao huongeza rutuba ya udongo na husababisha ongezeko la mavuno.
Faida
Hudhibiti wadudu na magonjwa shambani ambao hushambulia mazao mahususi.
Mimea ya jamii ya kunde huongeza nitrojeni kwenye udongo, na hivyo kuhuisha udongo na kusawazisha rutuba ya udongo.
Mpango wa mzunguko wa mazao
Tambua aina ya udongo iliyo shambani kwa kupima udongo au kupitia historia ya mazao yaliyopandwa awali ili kutambua ni aina yipi inayofaa kupandwa.
Angalia nyuma kuhusu historia ya uzalishaji wa mazao na kisha fanya kilimo mseto iwapo ni zao moja tu ambalo limekuzwa hapo awali.
Amua juu ya mpango wa kilimo wa muda mrefu unaoruhusu shamba lako kutolemewa.
Usifuatanishe mazao mawili yanayohitaji virutubisho vingi, kwa hivyo diama yafuatanishe na mazao yanayohitaji virutubisho vichache.
Panda mboga za mizizi kabla ya kubadilishana nafaka na kunde.
Usipande nafaka kwenye shamba hilo hilo, kila mara panda kunde au mboga kati ya mimea ya nafaka ili rutuba ya udongo irejeshwe.
Iwapo ardhi inatosha badilishana mashamba ya nafaka na mikunde ili kurutubisha udongo na kudhibiti magonjwa.
Iwapo ardhi haitoshi, panda mseto ili kudhibiti magugu, wadudu, pamoja na kuongeza rutuba ya udongo.