Vyama vya watumiaji wa rasilimali za maji (WRUA) huundwa na watumiaji wa maji, na wamiliki wa ardhi iliyo kando ya mito. Vyama hivyo huundwa kusimamia na kuhifadhi vyanzo vya maji vya pamoja.
Malengo yao makuu ni kupunguza mizozo kuhusu maji, kutoa mgawanyo sawa wa maji, na kulinda mazingira yaliyo kando ya mto, ambao hujulikana kama maeneo ya pwani.
Kuanzisha chama cha watumiaji wa maji
Nchini Kenya, vyama vya WRUA vilianzishwa miaka ya 1990‘s. Vinaanzishwa na jamii zilizo kando ya mito, na vinahakikisha ushiriki mwema wa wanachama katika maamuzi yote ya usimamizi na matumizi ya maji ya mto.
Utatuzi wa Mizozo
Mizozo hutatuliwa kupitia mgawanyo sawa wa rasilimali za maji kati ya watumiaji wa juu ya mto na wa chini. Asilimia 70% ya rasilimali za maji hupewa jamii, halafu 30% huachwa ili kulinda mazingira yaliyo kando ya mto. Ulinzi wa mazingira yaliyo kando ya mto hufanywa kupitia kufunza wanachama kuhusu kuhifadhi mimea iliyopo, pamoja na kupanda miti kwenye ardhi hiyo.
Ulinzi wa kisima hufanywa kwa kujenga ukuta ukizunguka mito ili kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na mporomoko wa matope. Uzoefu unaonyesha kwamba mazungumzo kati ya jamii ndio njia bora ya kutatua mizozo.
Manufaa za vyama vya WRUA
Vyama vya WRUA hutoa mgawanyo sawa wa maji, husaidia kutatua mizozo kati ya wadau, na kuboresha usimamizi wa ardhi na maji.