Kutopatikana au upatikanaji mdogo wa mbegu bora na aina bora za miwa ni kikwazo kikubwa kwa wakulima wa miwa.
Vipandikizi vya shina mbegu zinazotumika katika upandaji wa miwa kibiashara, na kila kipandikizi kinaweza kuwa na kichipukizi kimoja, viwili au vitatu. Uharibifu wa aina mbalimbali za miwa husababishwa na magonjwa, ukame, hali ya udongo n.k, jambo ambalo hupunguza mavuno. Mbinu maalumu ya kukuza mmea kwa kutumia kipande chochote cha mmea huo ambayo hujulikana kama tissue culture inafaa ili kuzidisha mbegu mpya kwa haraka. Kuhusu kukuza miwa, mbinu hii ni bora kwani hupunguza wingi na uzito wa nyenzo za miwa zitakazopandwa. Ili kupata mavuno mengi, hakikisha unatekeleza umwagiliaji kwa njia ya matone katika shamba lako la miwa.
Hatua za uzalishaji wa mbegu
Katika hatua ya kwanza, mbegu za miwa hupandwa kwenye kitalu. Mbegu za miwa huuliwa viini kwa kutumia viuatilifu. Hatua ya pili inahusisha kupandikiza mbegu kutoka kwenye kitalu cha awali na kuzipeleka shamba kuu. Uvunaji hufanywa kwa miezi 6–8 ili kukuza kitalu cha kibiashara.
Hatua ya tatu inahusisha kukuza kitalu cha kibiashara. Matibabu ya joto yakifanya kisiwe na magonjwa kwa takriban miaka mitano.
Tiba kwa joto
Maji ya moto, hewa yenye unyevunyevu na mvuke hutumika. Matibabu ya muda mrefu huhusisha matumizi ya kiwango cha 50 ° C cha maji moto kwa saa 2. Matibabu mafupi huhusisha matumizi ya maji moto kwa kiwango cha 52 ° C kwa dakika 20.
Katika matibabu ya mvuke, vipandikizi huwekwa kwenye chombo ambacho pia kuwekwa ndani ya kitengo maalum. Mvuke na hewa hupitishwa ndani ya kitengo cha matibabu, na vipandikizi hutibiwa kwa saa moja kwa 50 ° C , na mbinu hii nzuri sana dhidi ya magonjwa.
Kupandikiza miche
Mbolea ya NPK kwa uwiano wa 275:62.5:113.5 huongezwa kwenye kitalu. Ongeza 50kg ya nitrojeni na 75 Kg potasiamu mwezi mmoja kabla ya kuvuna miwa. Kupandikiza hufanywa wiki 4–5 baada ya kupanda vipandikizi kwa muachano wa 90cm kwa 90 cm. Vipandikizi hutibiwa na mchanganyiko wa viuakuvu katika kila hatua.
Tumia viriba ya plastiki vya ukubwa wa futi 6 kwa futi 4 vilivyo na matundu madogo chini yavyo.