Kupitia mbinu bora za kilimo, maharagwe zaidi yanaweza kuzalishwa na hivyo kutoa chakula na pesa zaidi. Maharagwe ni chanzo muhimu cha chakula, na mapato kwa wakulima na familia nyingi.
Ingawa mbegu bora zilizothibitishwa ni ghali, huwa zinaota kwa urahisi, na huboresha mazao. Ni muhimu kupanda maharagwe kwenye safu baada ya kutayarisha shamba kwa kusafisha, kulima na kulisawazisha: Tumia vijiti ili kuongoza upandaji wa maharagwe kwenye safu, huku ukifuata mwinuko wa ardhi. Ili kupanua mazao, fuata miongozo ya matumizi ya mbolea kutegemea aina ya udongo. Pia, palilia mimea katika wakati sahihi.
Kupanda kwenye safu
Tumia mbegu bora zilizothibitishwa kwani hizi huota vyema. Kufanya huku hupunguza magonjwa, huboresha mazao, na pia huokoa mbegu. Panda maharagwe katika safu ili kupunguza mmomonyoko wa udongo na ushindani wa virutubisho. Pia kunasaidia kurahisisha utambuzi wa wadudu na magonjwa waliyoko shambani, pamoja na kuokoa gharama za kazi. Tumia mchanganyiko wa mbolea ya UREA, DAP na mbolea ya kuku ili kuongeza mazao. Palilia shamba mara 3, yaani wiki 3 baada ya kupanda na mara mbili kila baada ya wiki 2.