Umwagiliaji kwa njia ya kunyunyizia maji na kwa njia ya matone huokoa maji, lakini gharama zake ni kubwa. Kwa hivyo, teknolojia mpya zimebuniwa.
Umwagiliaji kwa njia ya mtungi ni mbinu ya bei nafuu ambayo huokoa maji na hutumiwa kukuza matunda na mboga katika maeneo kame. Katika umwagiliaji kwa njia ya mtungi, mitungi huzikwa kwenye udongo na hujazwa na maji. Maji huvuja polepole kupitia kuta za mtungi yakielekea kwenye mizizi ya mmea. Umwagiliaji kwa njia ya mtungi ni muhimu sana kwa mazao yaliyokuzwa katika udongo wenye chumvi.
Faida za umwagiliaji kwa njia ya mtungi
Njia hii hutumika kukuza mimea kwenye miteremko mikali na maeneo ambapo umwagiliaji wa kawaida haufanyiki. Kuna magugu machache katika umwagiliaji kwa njia mtungi kwa vile maji hutolewa kwenye mizizi pekee. Umwagiliaji kwa njia ya mtungi sio ghali kuanzisha, na ni rahisi kutumia.
Ujenzi wa mitungi
Chagua mitungu ya takriban lita 10 ambayo hutengenezwa kwa udongo na kuwashwa kwenye moto mkali au tanuru. Kuta za mtungi lazima ziwe na unene wa 1cm. Chimba shimo la mviringo ili mtungi unapowekwa kwenye udongo, shingo yake itakuwa juu ya udongo.
Weka mtungi ndani ya shimo na ujaze nafasi iliyo kati ya mtungi na shimo kwa udongo uliochanganywa na samadi iliyooza. Kisha jaza mtungi maji na uufunike.
Kila mtungi huongeza unyevu kwenye udongo hadi 40cm kutoka kwenye mtungi. Katika shamba la mboga, zika mitungi kwa umbali wa cm 40 kutoka kwa kila mmoja. Katika minazi, acha cm 60 hadi 90 kati ya mtungi na shina. Kwa miembe, acha umbali wa sentimita 50 hadi 75 kati ya mtungi na shina kuu. Kwa miti ya matunda iliyokomaa, ambayo pia ilipandwa kwa umbali wa mita 4, weka mtungi katikati ya miti 2.