Kwa kuwa ni jambo muhimu la ukuaji wa mazao, kiwango cha umwagiliaji kinaamuliwa na aina ya mazao, msimu na uwezo wa mkulima kununua vifaa.
Umwagiliaji kwa njia ya matone hutumia mabomba ya plastiki ambayo huwekwa juu ya ardhi au ndani ya ardhi ili kutonesha maji, na pia kupunguza uvukizi wa maji na hivyo kuboresha ukuaji wa mazao.
Kufunga mfumo
Mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone huhitaji shinikizo la pauni 10-20 kila inchi ya mraba ya maji. Tumia chujio katika mfumo wa matone ili kuzuia matundu ya umwagiliaji kuziba kwani hii pia huchuja uchafu katika maji. Safisha mfumo mara kwa mara. hata hivyo, idadi ya njia za matone huamua ukubwa wa mstari kuu wa maji.
Vile vile, mabomba yanaweza kuwekwa juu ya ardhi au ndani ya ardhi kulingana na mazingira, uwepo wa magugu, na aina ya mazao. Katika hali hii, mabomba yanaweza kuwekwa inchi 5 chini ya ardhi. Mabomba yaliyowekwa juu ya ardhi lazima yafunikwe ili kuwe na maji karibu na mimea iliyopandikizwa.
Mwishowe, mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone hukuruhusu mkulima kumwagilia eneo kubwa kwa kutumia kiwango kidogo cha maji.