»Ulinzi wa ukingo wa mto«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/riparian-zone-protection

Muda: 

00:08:31
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

WOCAT

Ukingo wa mito hulindwa kwa kupanda mimea kwenye ukingo, pamoja na maeneo yaliyo karibu na mito. Hii hudhibiti mmomonyoko wa ukingo, mporomoko wa ardhi na mtiririko wa mchanga katika mto.

Daima ni muhimu kwa wakulima kulinda kingo za mito kwa sababu huku kunazuia mmomonyoko wa ardhi, kunapunguza mtiririko wa maji na uharibifu wa mafuriko, na kuboresha maisha ya mkulima kwa sababu miti iliyopandwa hutoa kuni, mbao, lishe ya wanyama na matunda kwa familia.

Hatua za kupanda

Panda nyasi za napier katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kwani nyasi hustawi na hivyo kutunza udongo dhidi ya mmomonyoko.

Pia panda, miti ya mgrivea lakini usijaze shimo la kupandia na udongo ili liweze kukusanya maji yanayotiririka.

Panda miti ya mpera ukingoni mwa mito ikiwa ukingo umethibiti vyeme. Hizi hufanya msitu mzuri wa kulinda udongo, matunda yake yanaweza kuliwa na pia ni chanzo kizuri cha kuni.

Unaweza pia kupanda miti ya mianzi kwa ukingo ambapo kuna mtiririko wa mto wa nguvu.

Linda miti ya asili kwa sababu huwa inahifadi udongo na kudhibiti mmomonyoko.

Mwishowe tunza kingo za mito kupitia udhibiti wa magugu, kukata nyasi ya napier na kupogoa miti.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0002:02Ukingo wa mito hulindwa dhidi ya mafuriko kwa kupanda mimea kwenye ukanda
02:0302:10Hatua za kupanda
02:1103:36Panda nyasi za napier katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko
03:3704:10Panda, miti ya mgrivea lakini usijaze shimo la kupandia na udongo
04:1104:46Panda miti ya mpera ukingoni mwa mito ikiwa ukingo umethibiti vyeme
04:4706:14Panda miti ya mianzi kwa ukingo ambapo kuna mtiririko wa mto wa nguvu.
06:1507:21Linda miti ya asili
07:2207:43Dumisha hatu bora za utunzaji wa ukingo wa mto.
07:4407:55Manufaa za ulinzi wa ukingo wa mto.
07:5608:31Dhibiti mmomonyoko wa udongo ukingoni mwa mto, punguza uharibifu wa mtiririko wa maji, boresha maishilio ya wakulima.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *