Mbegu ni nyenzo hai na ubora wake hupungua wakati wa kuhifadhi. Tahadhari zinapaswa kuchukuliwa wakati wa kuhifadhi ili kupunguza kushuka kwa ubora.
Ubora wa mbegu wakati wa kuhifadhi hutegemea unyevu. Ikiwa mbegu hazijakaushwa vizuri kabla ya kuhifadhiwa, zinakuwa laini, moto na nyevu, jambo ambalo litasababisha magonjwa na mashambulizi ya wadudu, na baadae kusababisha ubora wa mbegu kushuka. Kutumia mbegu bora zaidi husaidia kupunguza kiwango cha mbegu kinachohitajika kupandwa, na hivyo kuongeza mavunomsimu unaofuata.
Mbegu bora
Ili kupata mbegu bora, chagua gunzi nzuri kutoka shambani. Zipukuchue na zikaushe kwenye meza, kisha ziweke kwenye chombo juu ya meza. Safisha na kausha vyombo vya kuhifadhia mbegu kabla ya kuvitumia. Vyombo vinavyotumika kuhifadhi mbegu ni pamoja na vyungu vya plastiki, makontena, mapipa. Iwapo vyungu vinatumiwa, hupakwa rangi ndani na nje kwa kutumia lami au mafuta ya kupikia yaliyotumika ili kuzuia hewa kuingia ndani ya chombo.
Ufungaji na uhifadhi
Baada ya kukausha vizuri, weka mbegu kwenye chombo hadi ukingoni. Ikiwa huna mchele wa kutosha, mchanga mkavu unaweza kutumika kujaza nafasi iliyobaki. Unaweza pia kuwasha mshumaa ndani ya chombo na kukifunika ili kuondoa oksijeni yote iliyondani ya chombo na hivyo kusababisha wadudu walio ndani kufa. Chini na juu ya chombo, unaweza kuweka tumbaku kavu au majani ya mwarobaini ili kudhibiti wadudu.
Weka vyombo juu ya ardhi ili kupunguza ukungu na wadudu.