Kwa kutumia dumu safi isiyopitisha hewa, maharagwe yanaweza kuhifadhiwakwa muda mrefu. Hata hivyo, dumu lazima lisiwe na vitu hatari kama vile mafuta au dawa.
Wadudu hutoboa mashimo kwenye maharagwe na hivyo hupunguza uzito, ubora na uwezo wa mbegu kuota. Hata hivyo, kuhifadhi mbegu kwenye dumu huua wadudu waharibifu wa maharagwe na hivyo huongeza muda wa maisha ya maharagwe kwa angalau miezi 6 ikiwa mbegu zitatumika kwa ajili ya kupanda, na muda usio na kikomo iwapo maharagwe yatatumika kwa chakula. Huku kunasababisha uwepo wa chakula kingi zaidi kwa mwaka mzima na huleta bei nzuri kwa wakulima.
Kuhifadhi maharagwe
Kausha na uchague maharagwe kwenye turubai ili kupunguza unyevu. Jaza maharagwe katika dumu. Ukubwa wa dumu unaweza kuanzia lita 10 kwa kilo 10 hadi lita 20 kwa kilo 20.
Tikisa na ujaze nafasi ya dumu ili kuhakikisha kuwa dumu limejazwa na maharagwe kwani iwapo kuna nafasi wadudu watayavamia.
Funga vizuri mdomo ya dumu na kifuniko kisicho na mashimo.
Andika tarehe ambapo ulifungua dumu na tarehe ambapo unatarajiwa kutumia maharagwe kwa kuwa maharagwe huhifadhiwa kwa muda wa miezi 6 tu. Hata hivyo, usifungue dumu kwa mwezi mmoja ili kuua wadudu waharibifu.
Kamwe usifungue dumu hadi maharagwe yatakapohitajika kutumika ili kuzuia uingizaji wa hewa ambayo inaweza kuwezesha wadudu waharibifu kuangua mayai.