Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi- cassava mosaic virus

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/cassava-mosaic-virus

Muda: 

00:11:40
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Songhaï Centre

Barani Afrika, muhogo ni moja wapo ya mazao makuu yanayolimwa kwa kiasi kikubwa kwa chakula na mapato, kwa wakulima na wazalishaji.

Ugonjwa wa batobato ni moja wapo ya magonjwa muhimu ambayo huathiri uzalishaji.

Dalili za ugonjwa

Ugonjwa huo husababishwa na virusi vya muhogo vinayosambazwa na nzi weupe.

Mimea yaliyoathiriwa na ugonjwa huo inaweza kutambuliwa kwa madoadoa/ mabaka mepesi ya kijani au manjano kwenye majani. Pia, kwa majani madogo na yaliyoharibika.

Ugonjwa huo hauna tiba lakini unaweza kudhibitiwa.

Udhibiti wa ugonjwa

Tumia vipanda vya mihogo kutoka kwa wazalishaji waliothibitishwa. Panda aina za mihogo zinazostahimili magonjwa. Fanya kilimo cha mzunguko wa mazao ili kukomesha mzunguko wa magonjwa. Ng‘oa na kuchoma mimea yote yaliyoathiriwa na ugonjwa.

Panda aina moja shambani kwa wakati mmoja.

Daima, kagua shamba lako kwa ushambuliaji wa magonjwa.

Epuka kutumia vipanda vilivyoathiriwa wakati wa kuanzisha shamba.

Chukua vipanda kutoka kwa wazalishaji na wakulima waliothibitishwa.

Pata ushauri kutoka kwa watoa huduma wa ushauri. Mafunzo hutolewa na mashirika ya utafiti.

 

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:32Ugonjwa wa batobato ni moja wapo ya magonjwa muhimu ambayo huathiri uzalishaji.
01:3202:53Mimea yaliyoathiriwa na ugonjwa huo inaweza kutambuliwa kwa madoadoa mepesi ya kijani au manjano kwenye majani. Pia, kwa majani madogo na yaliyoharibika
02:5403:39Ugonjwa huo husababishwa na virusi vya muhogo vinayosambazwa na nzi weupe
03:4604:26Idadi nyingi ya nzi weupe hudumisha ugonjwa
04:2704:52Vipanda pia vinaweza kusambaza ugonjwa
04:5305:49Tumia vipanda safi
05:5006:04Chukua vipanda kutoka kwa wazalishaji na wakulima waliothibitishwa
06:0506:39Pata ushauri kutoka kwa watoa huduma wa ushauri
06:4008:15Panda aina za mihogo zinazostahimili magonjwa
06:4008:15Fanya kilimo cha mzunguko wa mazao kama vile mahindi, karanda, au mawele baada ya kupanda mihogo.
08:1609:46Panda aina moja shambani kwa wakati mmoja. Daima, kagua shamba lako kwa ushambuliaji wa magonjwa
09:4711:40Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *