Mchakato wa kukuza samaki unahitaji mbinu maalum. Hata hivyo, samaki hufugwa kwa kutumia mbinu tofauti.
Ufugaji wa samaki unahusisha kushughulikia na kukuza samaki kwenye matangi na vizimba ili kutoa chakula kwa watu. Aina za samaki zinazotumika ni pamoja na; tilapia, cat fish na aina nyinginezo. Nyavu hujengwa pande zote na chini ya kila tanki. Samaki dume huvutia samaki jike kwenye kiota chake ili kutaga mayai ambayo dume hurutubisha.
Kukuza samaki
Mayai huvunwa kwa kutumia nyavu na kisha kuhamishiwa eneo maalum ili kuanguliwa kuwa samaki wachanga. Maji huongezwa kwenye eneo la kuangulia mayai ili kuandaa hali iliyo sawa na ile ya mfumo wa mto ambayo inahitajika kwa kuanguliwa.
Samaki wachanga huchukuliwa kwenye matangi baada ya wiki sita, ambapo huhifadhiwa kwa muda wa miezi 2. Uwiano wa malisho ambayo hutolewa kwa samaki hulinganishwa na ukuaji wa samaki, yaani samaki hulishwa kulingana na uwiano wa uzito wa mwili wake.
Samaki hulishwa mara 3 kwa siku na ubora wa maji hupimwa kila siku mara 3 ili kuepuka vikwazo kwenye mfumo.
Mara samaki wanapokuwa wakubwa, basi huchukuliwa kwenye tanki maalum hadi wawe tayari kuvunwa. Samaki huvunwa kati ya miezi 6 hadi 8 wakiwa wamefikisha uzito wa 300–350g.
Samaki huchukuliwa na kupimwa kila baada ya wiki 2 na kila tanki la kukuzia samaki huwekwa alama ya tarehe ya samaki kuzaliwa.