Ufugaji wa kuku una manufaa makubwa ila magonjwa ni changamoto kubwa. Iwapo magonjwa yatadhibitiwa vyema na ndege kulishwa vizuri, mradi huo hutoa mapato mazuri kwa muda mfupi.
Faida za ufugaji wa kuku ni pamoja na, kuongeza mapato, fursa za ajira, na chanzo cha mbolea ya nitrojeni. Ili kupata matokeo mazuri, ndege wanapaswa kupewa malisho bora kwa wakati ufaao. Kwa mfano, wape malisho ya awali kwa muda wa wiki 4–5 na malisho ya kumalizia kwa wiki nyingine 3. Jua kwamba kadiri idadi ya kuku inavyoongezeka ndivyo kipato kinavyoongezeka. Hakikisha kuna jenereta kwa ajili ya kulisha ndege mara kwa mara ili kuongeza mapato kwa muda mfupi.
Usimamizi na zana
Daima tumia maji ya kunywa yaliyotibiwa yasiyo na harufu mbaya, ambayo yana ph sahihi kati ya 6 na 7.5. Changanya maji haya na chanjo asubuhi mapema ili kuepuka joto kali la wakati wa mchana. Hakikisha unachanja kuku ili kidhibiti magonjwa.
Pili, usiwape kuku maji kwa muda wa saa 1 ili chanjo itumike kikamilifu. Usichanganye ndege kutoka vyanzo tofauti ili kuepuka kueneza magonjwa. Kuku wanapaswa kupewa maji yaliyo katika hali joto ya 10–14 C. Kiwango cha kuhifadhi ndege kinapashwa kuwa kilo 25 katika eneo la mita moja wakati wa kuchinjwa.
Hatua za usalama wa ndege
Anza kwa kulizungushia uzio shamba, kisha safisha banda la kuku hasa wakati wa kuingiza kundi jipya. Pia ua viini kabla ya kuingia kwenye banda ili kuzuia kueneza magonjwa kwa mifugo. Dhibiti wadudu wanaovamia shamba kwani hawa ni wabebaji wa magonjwa.
Hatari na changamoto
Magonjwa, hii ni hatari kubwa kwani husababisha vifo vingi. Hata hivyo, magonjwa yanaweza kudhibitiwa hasa kupitia kanuni sahihi za usimamizi. Ukosefu wa fedha za kutosha huleta changamoto kubwa kwa ufugaji wa kuku kwani biashara hiyo inahitaji fedha. Wafugaji hutumia takiribani 70% ya fedha katika ununuzi wa malisho.