Kanga ni ndege wanaotoka barani Afrika, na wakati mwingine huitwa guineas, pintaids au gleanies. Ni ndege sugu sana, wenye nguvu na hawakabiliwa sana na magonjwa, na hufugwa kwa ajili ya nyama na mayai.
Kuanzisha ufugaji wa kanga kunahitaji mtu: kuangalia kanuni za eneo ili kuhakikisha kufuga ndege wa porini kunaruhusiwa; na kuchagua eneo zuri lenye mahitaji yote kama vile maji safi, hewa safi na bila uchafuzi. Ununuzi wa vifaranga ni jambo muhimu kwa mafanikio ya biashara ya ufugaji wa kanga. Pia nunua vifaranga wakiwa wawili, yaani jike na dume. Hifadhi ndege ndani ya banda kwa wiki 1–2 baada ya kuwanunua ili kuwawezesha kuzoea mazingira mapya.
Faida za kanga
Kushughulikia na kutunza kanga ni rahisi, huhitaji nafasi ndogo ya makazi na, na hivyo gharama za makazi ni kidogo. Pia, hawashambuliwi sana na magonjwa, ni rahisi kulisha na tija yao ya kibiashara ni juu sana.
Ndege kanga hupendelewa sana kwa sababu wanaweza kudhibiti wadudu kama vile kupe, nzi, panzi na nzige kwa kuwala. Hatimaye, huzuia panya kuvamia eneo.
Kulisha ndege na kuandaa makazi
Ndege kanga hupenda kuzurura huria na kujitafutia chakula. Kanga hula aina mbalimbali za wadudu, mbegu za ngano, konokono na minyoo. Pia huhitaji mboga za majani kwa ajili ya kudumisha usagaji chakula, na hivyo hula nyasi na magugu.
Ndege kanga huhitaji huduma chache za makazi. Takriban futi za mraba 2–3 za nafasi zitatosha kila ndege, sakafu nzuri iliyofunikwa na nyenzo kama vile maranda ya mbao, nyasi au majani.
Kuzaliana na mahitaji ya lishe
Kwa ujumla dume mmoja hufugwa na jike mmoja, lakini dume mmoja anaweza kupandana na majike 5–6. Iwapo jike ataacha kiota chake kabla ya kuangua, hamishia mayai kwenye mashine ya kuatamia. Kipindi cha kuatimia ni kati ya siku 26–28.
Kanga huhitaji kiwango cha juu cha protini. Kiwango cha protini cha 4–26% ni kizuri kwa vifaranga, na hupunguzwa hadi 18–20% katika wiki ya 5–8. Baada ya wiki 8, vifaranga hulishwa 16% ya chakula cha ndege ya mayai.