»Udhibiti wa magugu katika mpunga»

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=Sp6HLYq8Qqs

Muda: 

00:17:00
Imetengenezwa ndani: 
2012

Imetayarishwa na: 

africaricecenter

Magugu ni changamoto kubwa kwa wakulima wa mpunga kwa sababu hufanya utayarishaji wa shamba kuwa mgumu, hushindania maji na virutubisho, na hivyo kupunguza mavuno. Magugu mawili makuu ni pamoja na ; magugu ya kudumu na magugu ya kila mwaka.

Katika nyanda za chini, panda kwa umbali wa 15cm. Iwapo unapanda shambani moja kwa moja, palilia baada ya wiki 3. Kwa mpunga uliyopandikizwa, kupalilia mwanzoni mwa kutoa matawi. Ongeza naitrojeni ili kupanua mavuno.

Hatua za udhibiti

Lima na sawazisha shamba, kisha furika mpunga. Kulima kunasaidia kuzika magugu kwa kina na hivyo magugu hushindwa kuota. Kulima pia huondoa magugu ambayo hukauka baadaye.

Furika shamba lililosawazishwa kwa muda wa wiki 2 ili kuua magugu yaliyopo.

Lima na ufurike shamba mara ya pili ili kuua magugu yote kwa vile yanaweza kuota kwa mbegu na mizizi.

Safisha mifereji ya umwagiliaji na kingo za shamba. Suuza mifereji ya umwagiliaji ili kuepuka kuingiza mbegu za magugu kupitia maji na upepo.

Tumia mbegu zenye afya, zilizokaushwa vizuri na zilizohifadhiwa vizuri, zisizo na magugu kwa uotaji mzuri wa mbegu na mimea yenye nguvu.

Chagua aina nzuri, tumia vipandikizi na muachano unaofaa ili kuwezesha mimea kustahimili magugu.

Tunza maji kiasi shambani ili kuzuia uotaji wa magugu.

Toa maji shambani na uweke mbolea au dawa ili kuwezesha ukuaji wa haraka, na kudhibiti magugu.

Panda kwa safu ili kubainisha magugu na mpunga kwa urahisi, na hivyo kudhibiti magugu.

Tumia dawa ya kuua magugu baada ya kuuliza muuzaji au mshauri.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:15Udhibiti mzuri wa magugu hupanua mavuno ya mpunga
01:1604:07Magugu mawili makuu ni pamoja na ; magugu ya kudumu na magugu ya kila mwaka
04:0804:55Hatua za kudhibiti magugu
04:5605:17Lima na sawazisha shamba ili kuandaa shamba.
05:1805:48Furika shamba lililosawazishwa kwa muda wa wiki 2
05:4907:47Lima na ufurike shamba mara ya pili
07:4808:16Safisha mifereji ya umwagiliaji na kingo za shamba. Suuza mifereji ya umwagiliaji.
08:1709:11Tumia mbegu zenye afya, zilizokaushwa vizuri na zilizohifadhiwa vizuri, zisizo na magugu.
09:1210:50Chagua aina nzuri, tumia vipandikizi na muachano unaofaa
10:5111:23Tunza maji kiasi shambani, ongeza mbolea na tumia dawa ya kuua magugu.
11:2412:07Ng‘oa magugu kwa mkono, zana au dawa. Panda katika mistari.
12:0812:32Palilia shamba baada ya wiki 3 na baada ya wiki 2–3 kwa mbegu zilizopandwa moja kwa moja.
12:3313:28Kwa mpunga uliopandikizwa, palilia tu mwanzoni mwa kutoa matawi, na uweke mbolea ya nitrojeni.
13:2914:23Tumia dawa ya kuua magugu baada ya kuuliza muuzaji au mshauri.
14:2417:00Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *