Kilimo mjini ni muhimu sana kwa wakulima katika miji kwa kuwa ni chanzo cha mapato. Miji hiyo ina maji mengi na taka amabazo zinaweza kubadilishwa kuwa chakula na faida, lakini kinachokosekana ni nafasi.
Ng‘ombe wa maziwa huhifadhiwa kwenye zizi na hupewa lishe humu. Hatua hii huitwa ufugaji wa ndani (Zero-grazing) na inafaa zaidi katika mahali ambapo ardhi ni adimu. Takataka za kikaboni zinaweza kuchakatwa kuwa lishe ya ng‘ombe. Matunda yaliyotupwa, mboga majani na maganda ya ndizi yanafaa kuchambuliwa kabla ya kutumiwa kama lishe.
Mfumo wa gesi ya kupikia (biogas)
Samadi ya ng‘ombe inaweza kubadilishwa kuwa gesi ya kupikia (biogas) ambayo husaidia kupunguza gharama ya stima, mafuta na pia kuboresha mazingira. Samadi ya ng‘ombe hukusanywa na kuwekwa kwenye kiingilio cha mtambo na kuchanganywa vizuri na maji huku nyasi na takataka zikitolewa. Hii kutoa mafuta kwa mtambo. Mchanganyiko huelekezwa kwa chemba kuu ambapo gesi ya methane hutolewa, na kisha kutumika jikoni. Mchanganyiko huo wa methane na kabondioksidi unaweza kutumika kwa kupikia na mwangaza. Mboji kutoka kwenye mtambo baada ya kuchacha unaweza kutumika kama mbolea kwa mboga, na matunda shambani. Mitambo ya bio gas yenye bei nafuu hupatikana sokoni. Hii ni njia nzuri ya kurejeleza rasilimali ambayo husababisha mazingira kubaki safi.