Uvunaji wa maji ya mitaro ya barabara unaweza kufanya tofauti kati ya kupata mazao au kukosa. Wakulima wamebuni mbinu tofauti za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, wakitumia njia za kitamaduni na kutumia ubunifu wa hivi majuzi.
Mbinu ya uvunaji wa maji ya mitaro ya barabara inaweza kugawanywa kati ya zinazotumia maji ya bomba, na zinazokusanya maji machache kutoka kwa barabara, zinazosambaza maji shambani na zile zinazokusanya maji kwenye mabwawa. Mikondo ya maji huongozwa kwa mifereji na miinuko ya udongo. Maji haya huenea katika shambani yakilowesha udongo uliyokauka pamoja na miti ya matunda.
Manufaa
Katika maeneo ya mvua nyingi, Uvunaji wa maji ya mitaro ya barabara unaweza kutekelezwa kwa kukusanya maji kwenye kidimbwi kilicho shambani, ambacho kinaweza kutumika kutolea maji mimea ya matunda na mboga.
Uvunaji wa maji ya mitaro ya barabara hutunza mazingira kwa kuzuia mmomonyoko wa udongo ambapo udongo wa juu unasafirishwa kwenda mtoni na kuacha mashamba bila rutuba. Pia husaidia kuongeza maji kwenye udongo.
Uvunaji wa maji ya mitaro ya barabara huongeza mazao shambani, na pia hufanya mimea kustahimili zaidi, na kuruhusu upanzi wa aina mbalimbali za mimea.