Usimamizi uendelevu wa ardhi hutoa msingi wa uzalishaji wa mimea, pamoja na kuthibitisha mfumo wa ikolojia, kutunza vyanzo vya maji na viumbe hai.
Usimamizi uendelevu wa ardhi hudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa kwa kukamata na kuhifadhi kaboni. Theluthi ya gesi zinazosababisha mabadiliko ya hali ya hewa hutoka kwenye kilimo, na mabadiliko ya matumizi ya ardhi. Mabadiliko ya hali ya hewa yanahusika na uharibifu wa ardhi. Wakulima wanahamasishwa kuwa wabunifu na teknolojia ili kupata suluhisho za mabadiliko haya. Wafadhili hukabili hali hii kwa kuchangia fedha zaidi ili kuboresha usimamizi uendelevu wa ardhi.
Mbunu za usimamizi wa ardhi
Mistari au mitaro ya mawe ni mfumo wa kuvuna maji ya mvua, ambayo hufanywa kwa kuweka mawe kwa ardhi iliyoteremka. Matuta ya Fanya juu husaidia katika uhifadhi wa udongo. Kilimo cha miti ya mgrivea, ambayo ni mti ya umuhimu anuai kinafanywa na wakulima wengi.
Uvunaji wa maji ya mvua yanayotiriri: Maji yanayotiririka kutoka barabarani yanaweza kuvunwa na kutumiwa kukuza mazao. Mbinu ya kufungia wanyama zizini na kutumia samadi yao kutengeneza biogesi ni moja wapo ya mbinu bora za usimamizi wa ardhi.
Mashimo ya Zai hukusanya maji, na yanafanya zaidi yanapoongezwa na mbolea, na kuwekwa kati ya mistari ya mawe. Mbinu ya demi lunes ni rahisi kuanzisha na hutumika kwa kukuza mazao, miti na malisho.
Kilimo cha kutawanya miti muhimu shambani huunda matawi yanayozuia upepo kubeba udongo. Usimamizi wa rutuba ya udongo kwa kutengeneza mashimo ya mbolea oza na kuongeza mbolea za madini kidogo.
Uhuishaji asili wa ardhi kupitia wakulima ni aina ya kilimo inayoruhusu mimea kuchipuka kutokana na mbegu au miti. Uhusiano mzuri kati ya wakulima na wafugaji ambao huwawezesha wote kufaidika. Mifugo hupata malisho, na mimea hupata samadi. Kilimo cha uhifadhi ni kizuri kwa wakulima wadogo.