Kuku ni chanzo cha protini na kipato kwa wafugaji, hata hivyo ugonjwa wa kideri huwaangamiza ndege haraka. Kwa hivyo utunzaji mzuri na kufuata hatua zinazopendekezwa unahitajika.
Kinyesi cha kuku hutumiwa kama mbolea ya kikaboni baada ya kuoza. Vifaranga hupenda kula mchanga na mkaa kwa usagaji wa chakula kwa urahisi. Epuka kuzaliana kati ya kuku walio katika familia hiyo hiyo, kwani huku kunaweza kusababisha kuku dhaifu. Weka vijiti kimlalo juu ya sakafu ili ndege waweze kupumzikia usiku na kukusanya kinyesi kwa urahisi.
Hatua za utunzaji
Jenga banda la kuku ili kuwalinda dhidi ya ndege wawindaji, wezi na hali mbaya ya hewa. Safisha banda mara kwa mara ili kuku waweze kuwa na afya bora. Nyunyiza majivu sakafuni ili kupunguza kushambuliwa na vimelea vidogo kama utitiri na kupe. Weka pumba za mbao au nyasi kavu ili kuandaa eneo la kutaga mayai, na pia kupunguza kushambuliwa na vimelea.
Udhibiti wa vimelea
Kuku anapotaga mara mbili, nyunyizia masanduku ya kutagia kwa acaricide, na majivu ili kudhibiti vimelea. Daima, funga ndege wadogo wakati wa wiki za kwanza ili kuwalinda dhidi ya wanyama waharibifu na kupotea. Wotolee vifaranga joto katika siku za baridi ili kudhibiti kifo. Unaweza hata kuwapa mchanganyiko wa ngano, shayiri, mahindi na majani kwa kuwa ni nafuu. Safisha vyombo vya maji kila mara na wape maji safi ili kuepuka magonjwa. Ongeza dawa za kienyeji kama vile majani ya mshubiri, pilipili kwenye maji ya kunywa ili kuimarisha kinga ya kuku dhidi ya magonjwa. Wazike ndege waliokufa ili kuepuka kuambukiza kuku wenye afya.