Makadamia au karanga pori ni zao muhimu kwa ajili ya mafuta yake yenye faida ambayo husaidia kuimarisha afya zetu.
Uzalishaji na usindikaji
Anzia kwenye kitalu kwa kuchagua aina za mbegu zinazohitajika na uzipandikize ili kutoa miche bora. Panda miche kwenye udongo usio na maji mengi, kwenye mteremko kwa muachano sahihi.
Baada ya kupanda, tunze miti kwa kuweka mbolea, kupalilia na kumwagilia maji katika nyakati za awali. Baada ya kuanzishwa, makadamia hustahimili hali ya ukame lakini unaweza kumwagilia maji ili kudumisha kiwango cha uzalishaji na ubora wa juu.
Mti wa makadamia unaotunzwa vizuri huanza kutoa karanga wakati miaka 4, lakini mavuno mazuri huanza baada ya mwaka wa 5. Fanya vipimo vya ukomavu kabla ya kuvuna. Wakati wa kuvuna, weka karanga kwenye mifuko safi. Pima uzani wa karanga, na kisha pakia mifuko kwenye matrela safi na kusafirishwa kiwandani.
Zikifika kiwandani, karanga hukatwa maganda, na kukaushwa hadi kufikia kiwango cha unyevu wa 10%. Kisha karanga hupelekwa kwenye kituo cha kupasuliwa ambapo unyevu hupunguzwa zaidi hadi 1.5% kabla ya kupasuliwa. Baadaye, bidhaa hiyo hupakiwa na ni tayari kuuzwa nje.
Kutoka kwa usindikaji wa makadamia, tunapata maganda ambayo yanaweza kuoza kuwa mbolea na kurudishwa shambani. Maganda pia yanaweza kutumika kama kuni.