Ufugaji wa kuku ni biashara yenye faida kwa kuwa bidhaa zake zinahitajika sana na hutoa faida kwa haraka. Hata hivyo, kabla ya kuwekeza kwenye ufugaji wa kuku kwanza tambua aina ya kuku unayoipenda.
Kawaida, kuku wa mayai huanza kutoa mayai kutoka wiki 18–19 hadi wiki 72–78. Kuna sekta kuu tatu za biashara ya kuku na hizi ni kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wanaofugwa huria. Zingatia sifa kuu za banda bora la kuku kama vile eneo kubwa, uwezo wa kuzuia mvua, usalama, kuta laini, uingizaji wa hewa, sakafu ya saruji na uwezo wa kuzuia panya. Inashauriwa kuanza na idadi ndogo ya ndege na kushauriana na daktari wa mifugo.
Mifumo ya usimamizi
Daima wape kuku wanaofugwa huria na chakula cha mkusanyiko, na wape kuku wa mayai chakula chenye lishe bora.
Pia hakikisha upangaji sahihi ili kutambua kwa urahisi mahitaji ya kimsingi yanayohitajika na mtaji kabla ya kuanza.
Zaidi ya hayo, hakikisha kuna uingiza mzuri wa hewa katika banda la kuku, weka matandiko ndani ya banda ili kutoa joto, faraja pamoja na kunyonya unyevu kutoka kwa kinyesi.
Panda malisho ya ziada au ununue milisho kutoka kwa wauzaji wanaotambulika, na haya lazima yachachushwe kwa siku 3 ili kupunguza gharama za kulisha.
Hakikisha unasafisha vifaa kwa kutumia maji safi na ujifunze kuhusu sheria zinazoongoza jamii ili kupata mwongozo wa eneo.
Mara kwa mara nyunyiza dawa kwenye banda la kuku, toa kinyesi cha kuku na safisha banda la kuku.
Badilisha ndege wazee na ndege wachanga wenye sifa nzuri kwa uzalishaji endelevu.
Hatimaye, epuka msongamano wa ndege na zungushia banda uzio kwa ajili ya usalama.
Usimamizi wa vifaranga
Andaa eneo pa kushughulikia vifaranga mapema, pata viuavijasumu na uwape vifaranga maji wanapofikishwa bandani ili kudhibiti upungufu wa maji mwilini. Pia toa chanzo cha joto kwenye chumba cha kushughulikia vifaranga na hakikisha kuwa vifaranga hufanya mazoezi.
Wape ndege chakula chenye lishe kwa viwango vinavyofaa na udhibiti wanyama wawindaji.