Nyanya ni mojawapo ya mboga zinazotumiwa ulimwenguni kote, lakini huathiriwa na magonjwa mengi. Mnyauko bakteria wa nyanya ni ugonjwa mkuu wa nyanya.
Mmea wa nyanya unapoathiriwa na mnyauko wa bakteria, huanza kunyauka lakini majani hubaki mabichi. Shina linaweza kuonekana lenye afya nje lakini litakuwa linaoza ndani. Ikiwa shina la mmea ulioambukizwa hukatwa na kuwekwa kwenye glasi ya maji safi, dutu ya maziwa hutoka kwenye shina. Majimaji haya meupe ni bakteria wanaosababisha mnyauko.
Udhibiti wa mnyauko bakteria
Unapoona mnyauko, jambo bora zaidi ni kung‘oa na kutupa mmea ulioathirika mbali na shamba ili kuzuia uenezaji wa maambukizi kutoka mmea huo.
Kuua viini vilivyo udongoni kabla ya kupanda kunaweza kusaidia kuua bakteria wanaosababisha mnyauko wa nyanya.
Minyoo fundo husababisha vidonda kwenye mizizi ya mimea ambavyo bakteria hupitia kushambulia mizizi. Utumiaji wa dawa za kuua minyoo fundo husaidia kudhibiti mnyauko bakteria.