Kiduha ni gugu la kimelea ambalo hukua katika udongo ulio na rutuba duni. Lakini kupitia usimamizi jumuishi na mbinu kadhaa za kurutubisha udongo, gugu hilo linaweza kudhibitiwa.
Linapokua, kiduha hujishikamanisha kwenye mizizi ya mimea na hufyonza virutubisho na maji, na hivyo kuzuia ukuaji mzuri wa mimea. Mbegu za kiduha hutawanywa kwa urahisi kupitia mawakala wa mmomonyoko.
Hata hivyo, kilimo mseto cha mikunde na nafaka hupunguza uvamizi wa kiduha. Pia kungoa kwa mikono kabla ya kiduha kuchanua maua husaidia katika udhibit mtawanyiko wa mbegu zake.
Kiduha na usimamizi wa rutuba ya udongo
Kwanza, unapaswa kujua jinsi striga huishi ili kuelewa vyema mbinu za udhibiti wake. Pili, boresha rutuba ya udongo kwa kuweka mboji kwani huhifadhi unyevu na kurutubisha udongo. Panda mseto wa mazao, ngoa kiduha kwa mkono, na uwe mwangalifu kila wakati. Mikakati jumuishi ya udhibiti hupunguza uvamizi wa haraka. Mwisho, fanya juhudi za jamii katika udhibiti wa kiduha kwa kuungana na wakulima wengine ili kudhibiti kiduha na kuzuia kuenea kwa mbegu zake.