»Mfumo wa kukamulia unaojiendesha«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=ru2m8XNGICM

Muda: 

00:08:37
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Digital Agriculture

Wafugaji wa ng‘ombe wa maziwa hutumia teknolojia zilizoboreshwa kwa mfano mfumo wa kukamulia unaojiendesha, ambao ni muhimu sana kwa wakulima na wanyama.

Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa wanapaswa kukamua mara tatu kwa siku kwani huku huongeza uzalishaji wa maziwa na hupunguza mafadhaiko kwa wanyama. Mfumo huo hutambua mabadiliko iwapo kumetokea magonjwa au majeraha.

Faida za mfumo

Mfumo huo huwezesha uzalishaji wa maziwa safi, na hivyo kukidhi mahitaji ya watumiaji.

Pia mfumo huo humwezesha mkulima kutambua ugonjwa wa kiwele, na hivyo kuudhibiti kuenea.

Mfumo huo huhakikisha usafishaji wa maziwa na hivyo basi kuzuia magonjwa.

Mfumo huo vilevile unawezesha kurekodi uzalishaji wa maziwa kwa kutumia kompyuta, na hivyo kuboresha ufugaji wa ng’ombe.

Pia mfumo huo huharakisha ukamuaji wa ng’ombe na vile vile hupunguza matukio ya majeraha kwa matiti.

Wakulima walio na mfumo huo huokoa gharama ya wafanyikazi na pia hugundua kiwango cha uzalishaji wa maziwa kwa kila mnyama.

Mwishowe, mfumo huo husajili historia ya uzalishaji wa mnyama binafsi, na hivyo kumwezesha mfugaji kugundua mabadiliko katika uzalishaji, na hivyo kumshughulikia ifaavyo.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:12Faida za kutumia mfumo wa kukamulia unaojiendesha.
01:1301:40Mfumo huo huwezesha uzalishaji wa maziwa safi
01:4102:14Pia mfumo huo humwezesha mkulima kutambua ugonjwa wa kiwele
02:1503:20Mfumo huo huhakikisha usafishaji wa maziwa
03:2104:31Mfumo huo vilevile unawezesha kurekodi maziwa kwa kutumia kompyuta.
04:3205:35Pia mfumo huo huharakisha ukamuaji wa ng’ombe
05:3606:07Hupunguza matukio ya majeraha kwa matiti na huokoa gharama ya wafanyikazi.
06:0806:42Hugundua kiwango cha uzalishaji wa maziwa kwa kila mnyama.
06:4208:37Ng‘ombe wa maziwa wanapaswa kukamua mara tatu kwa siku. Mfumo huo husajili historia ya uzalishaji wa mnyama binafsi

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *