»Mfumo jumuishi wa kufuga bata wa mpunga | Mfumo endelevu wa kilimo hai«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=hde6k1b9HOA

Muda: 

03:17:00
Imetengenezwa ndani: 
2022

Imetayarishwa na: 

Discover Agriculture

»Mfumo jumuishi wa kufuga bata wa mpunga | Mfumo endelevu wa kilimo hai«

Mbinu hii ya kilimo hiki kinahusisha mfumo jumuishi wa ufugaji wa bata na ulimaji wa mpunga katika shamba la mpunga. Bata huchochea ukuaji wa mimea huku wakitembea shambani la mpunga kwa kulainisha kitope, wakati samadi ya bata hurutubisha udongo kiasili.
Bata hao pia hula wadudu waharibifu na magugu na hivyo kuondoa uhitaji wa dawa za kuulia wadudu na magugu. Kulingana na majaribio yaliyofanywa kwenye zaidi ya mashamba 1000 ya jumuishi la bata na mpunga nchini Ufilipino, kumekua ongezeko la tija ya mpunga hadi tani 9 kwa hekta. Nakadhalika, gharama za uzalishaji zimepungua kwa asilimia 30%. Pia mbinu hii imewezesha ukuaji wa biashara za kilimo kama vile mashamba ya bata-mpunga, mashamba ya bata, viwanda vya kuangulia mayai, viwanda vya kusindika nyama ya bata na biashara za rejareja. Biashara hizo hutoa manufaa nyingine kama vile kuongeza tija, mapato na ubora wa maisha ya wakulima na wahusika wengine.

Mayai ya Bata

Mayai ya bata hukaa mabichi na safi kwa muda mrefu kwa sababu ya ganda lao nene. Pia yana mafuta ya omega-3 zaidi.
Watu ambao hawawezi kula mayai ya kuku kwa sababu ya mzio wanaweza kula mayai ya bata. Asilimia 80 hadi 90 ya bata jike hutaga yai moja kila siku. Mayai safi yanaweza kuwekwa kwenye kiatimio ili kuanguliwa baada ya siku 28 na kuuzwa kwa wafugaji wa bata.

Mfumo wa kilimo hai

Mfumo jumuishi wa ufugaji wa bata wa mpunga huondoa hitaji la mbolea za kikemikali na dawa za kuulia wadudu na magugu. Kutokana na kutotumia pembejeo za kikemikali, afya ya udongo huboreshwa kwa muda.
Majimaji ya samadi ya bata pia inaweza kukusanywa na kuchanganywa na maganda ya mpunga na kuuzwa kama mbolea.

Utoaji wa gesi ya hari

Asilimia 21% ya gesi chafuzi zinazotolewa kwenye angahewa duniani kote hujumuisha gesi ya methani ambayo hutolewa hasa na mashamba ya mpunga yaliyofurika. Hii ni kwa sababu mafuriko huzuia usambazaji wa oksijeni kwenye udongo na kuharakisha uozaji wa nyenzo za kikaboni zinazotoa gesi ya methani kwenye angahewa.
Uchunguzi nchini China unaonyesha kuwa ufugaji wa bata katika mashamba ya mpunga hupunguza utoaji wa wa gesi chafuzi ya methani, na hivyo kuchangia katika kupunguza ongezeko la joto duniani.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:30Utangulizi wa ufugaji jumuishi wa bata wa mpunga na faida zake.
00:3101:00Kuongezeka kwa uzalishaji wa mpunga na ukuaji wa biashara za kilimo
01:0101:30Mayai ya bata hukaa mabichi na safi kwa muda mrefu kwa sababu ya ganda lao nene. Pia yana mafuta ya omega-3 zaidi
01:3102:00Ufugaji jumuishi wa bata wa mpunga kama mfumo endelevu wa kikaboni, huondoa hitaji la mbolea za kemikali na dawa za kuulia wadudu au dawa za magugu.
02:0102:30Jinsi mfumo jumuishi wa ufugaji wa bata wa mpunga unavyosaidia katika kupunguza uzalishaji wa gesi chafu katika angahewa.
02:3103:17Majimaji ya samadi ya bata hukusanywa na kuchanganywa na maganda ya mpunga na kuuzwa kama mbolea.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi