Mbinu ya kukata na kunyinyizia ni njia rahisi ambayo inaweza kutumika katika usimamizi wa misitu.
Mbinu hiyo inaweza kutumika kudhibiti aina za miti zisizopendekezwa, na pia huboresha makazi ya wanyamapori ambapo lengo ni kutoa malisho kwa mifugo. Huku kunafanywa kwa kufungua mwavuli wa msitu ili mwanga wa jua uweze kupenya hadi ardhini na hivyo kuruhusu mimea kukua. Mbinu hiyo pia husaidia kudhibiti aina vamizi za mimea.
Nyenzo zinazohitajika
Ili kutekeleza mbinu ya kukata na kunyinyizia, unachohitaji ni shoka ndogo kukata mti na chupa ya kunyunyuzia.
Kemikali zinazotumika katika mbinu hii ni pamoja na Imazapyr, Glyphosate na Triclopyr. Baadhi ya kemikali haziruhusiwi kutumika katika baadhi ya maeneo, kwa hivyo unahitaji kujua taarifa hiyo kuhusu kemikali zinazokubalika katika eneo lako kutoka kwa wakala wa ugani.
Unapoweka kemikali, hakikisha kuwa una vifaa vya kujikinga kama vile miwani, glavu, mashati ya mikono mirefu na suruali.
Utaratibu
Ili kutekeleza mbinu ya kukata na kunyunyizia, kanuni za kimsingi za kufuata ni kufanya mkato 1 kwa kila inchi 2 za kipenyo. Fanya mkato kwenye gome la mti kuingia ndani ya mti. Hii huhakikisha kwamba kemikali zinaingiza vizuri ndani ya mti.
Fanya mkato mmoja mzuri, fungua eneo lililokatwa na nyunyiza kemikali ndani.
Epuka kutumia mbinu ya kukata na kunyunyizia ikiwa mti uko karibu na nyaya za umeme au uzio au jengo au nyumba kwa sababu mti hatimaye hukauka na kuanguka.