Ili kutengeneza sileji bora unahitaji kuzingatia hatua katika michakato mbalimbali vile inavyoelezwa hapa chini. Uangalifu unapaswa kuchukuliwa wakati wa kujaza na kushinikiza sileji ili kila safu iwe na unene wa 15 – 30cm.
Epuka uchafuzi wa vifaa ili kudumisha ubora wa sileji.
Kutengeneza sileji
Chagua na panda mazao ambayo yanaweza kustahimili hali ya eneo lako, na ambayo yana uwezo wa kutoa mavuno mengi.
Zingatia muda sahihi wa kuvuna, na pia zingatia urefu mahsusu wa kukata mmea; kwa mfano kata nyasi kwa urefu 5cm – 10cm na, 15 – 30cm kwa mahindi.
Kata nyenzo kwa urefu wa 10mm – 20mm, kwa sababu nyenzo ndefu huwa ngumu kufungasha na huingiza hewa, na nyenzo fupi hutatiza kati kumeng’enya.
Weka nyenzo zilizokatwa katika eneo wazi ili kukausha maji ya ziada yaliyomu kabla ya kufanya mchakato wa kuhifadhi silegi ili kuzuia ukuaji wa ukungu.
Tumia chanjo zilizothibitishwa kama vile homofermentative na heterofermentative kudumisha viwango vya pH.
Jaza sileji, shinikiza na kufunika sileji kwa haraka ili kupunguza uwezekano wa kuingiza hewa ambayo husababisha ukuaji wa viumbe hai na uozo.
Funga vizuri ukitumia damani za plastiki ili kuzuia hewa kupenya ndani na kuharibu sileji. Hewa husababisha uozo na ukuaji wa ukungu.