Ikiwa unataka kuhifadhi mahindi kwa mda mrefu, sharti uyatunze vizuri.
Zingatia sehemu itakaotumiwa kuhifadhi mahindi dhidi ya wadudu. Kwa hivyo, hakikisha kwamba sehemu hii haingizi hewa.
Maghala ya Udongo
Tunafaa kutumia maghala ya udongo ili kuzuia mchwa, na kulinda mavuno vizuri. Maghala ya udongo hujengwa juu ya mawe ili kuzuia wadudu kama mchwa. Pia, ghalia hilo lina mifrege ya chini na vifuniko viwili. Kimoja cha udongo na kingine cha nyasi. Hivi husaidia kuzuia uvamizi wa wadudu.
Ni lazima na muhimu kusafisha ndani ya maghala ili yabaki safi na kavu. Tunafaa kuua viini kwa kuchoma nyasi kidogo ndani ya ghala na pia kutengeneza ukuta ulio pasuka ili kuhakikisha kila kitu kiko kwa utaratibu. Ikiwa unataka kuhifadhi mahindi yako kwa mda mrefu zaidi, unafaa kuongeza majani ya muarubaini.
Hatufai kueka mahindi mapya yalio vunwa pamoja na mahindi mengine ya msimu uliopita kwenye ghala moja. Nakadhalika, mahindi ya aina tofauti yasiwekwe pamoja kwasababu yaweza kuvamiwa.
Vituo vingine maalumu vya kuhifadhi mahindi
Unaweza kutumia ghala la chuma, mapipa na mifuko. Tumia magunia maalum ya PICS enye musito wamifuko mitatu: kuna mifuko miwili ya plastiki ndani, na sehemu ya nje iliyoshonwa na polypropylene. Kama hauna yoyote haya, basi tumia mifuko ya kawaida au gunia. Kisha unaweza kuongeza dawa za kutunza kwa sababu mifuko ya kawaida huingiza hewa.
Vitua vyote vyakuhifadhi mahindi havifai kugusa ukuta wala sakafu, na pia viweke juu ya magogo