Mbegu zilizo na madoa zina ugonjwa na zitakuletea mavuno yasiyosawa, na machache. Kwa hivyo ni vizuri kujua jinsi ya kuzitenganisha na mbegu zenye afya.
Ili kupata mavuno bora, unafaa kutumia mbegu nzuri na safi. Ni rahisi kutambua tofauti kati ya mbegu zilizo na madoa na mbegu zilizoshambuliwa na wadudu. Mbegu madoadoa ni zile ambazo zina madoa juu yake, na zile zilizoshambuliwa na wadudu zina mashimo.
Kusafisha mbegu
Ndani ya madoa kuna vijidudu vinavyojificha, kwa hivyo husababisha uharibifu baadaye. Hizi mbegu haziwezi kuondolewa kwa kupepeta wala kuelea, kwa sababu ni nzito kama mbegu zenye afya. Kwa hivyo lazima uziondoe kwa mkono.
Omba familia yako yote msaada. Hii hurahisisha kufanya kazi hiyo kwa kipindi kifupi. Kuchambua mbegu ni jambo la muhimu kwa sababu unapata pesa zaidi kwenye soko, na pia huboresha zao lako shambani.
Anza na kiasi kidogo cha mbegu safi za kupanda. Baada ya kupata mavuno mazuri, basi panda mbegu hizo safi kwa shamba lote. Unaweza kusafisha kilo moja ya mbegu na kuzipanda katika sehemu tofauti ya shamba. Baada ya kuvuna, begu zifuatazo zitasafishwa kwa urahisi zaidi kwa kupepeta tu. Ukiwa na kilo moja ya mbegu safi, utapata mbegu mpya nyingi safi.