Viwavijeshi ni wadudu hatari na waharibifu zaidi katika hatua ya mabuu(viwavi) katika mzunguko mzima wa maisha yao.
Mzunguko wa maisha yao ni pamoja na mayai, hatua 6 za ukuaji wa viwavi, kifukofuko na nondo.
Hii huanza wakati mayai 100 hadi 200 yanatagwa chini ya majani yaliyokaribu na msingi wa mmea, kwa sehemu ya makutano ya jani na shina.
Baada ya kuanguliwa, viwavi wachanga hula majani.
Viwavi hupendelea kula sehemu ambapo majani hukutana na shina katika mimea michanga, na pia hula majani yaliyo karibu na hariri za gunzi katika mimea iliyokomaa.
Viwavi hula maganda ya hindi, hadi kuingia ndani ya gunzi na huku huanza kula punje za mahindi.
Baada ya siku 14, Viwavi huanguka chini na kuchimba shimo la kina cha 2cm hadi 3 ardhini, ambamo wanaishi kama kifukofuko.
Siku 8–9 baadaye, nondo waliokomaa hutoka ardhini na kuanza mzunguko tena.