Mahindi ni chakula kikuu kwa sehemu nyingi za dunia pamoja na zao la kibiashara kwa wakulima na wafanyabiashara. Hata hivyo, ni muhimu kuwa na ujuzi na vifaa vya kutosha kuhusu mchanato wa kuvuna mahindi.
Kwa mahindi ambayo yako tayari kuvunwa, safu nyeusi hutengeneza kati ya punje, na gunzi na nafaka huhisi ngumu zinapobonyezwa. Kwa wakulima wanaovuna mapema hilo linapaswa kufanywa wakati hariri zinageuka kahawia, na kwa wale wanaochelewa kuvuna mmea unapaswa kuwa kavu kabisa.
Kuhakikisha mavuno sahihi
Vuna wakati mvua zimeisha ili mahindi yaweze kukauka kwa urahisi pia zungumza na mhudumu wako wa ugani kuhusu muda wa ukomaavu wa mahindi vile aina mbalimbali za mahindi huwa na vipindi tofauti vya kukomaa na kuhakikisha kuwa unaendana na muda wa kuvuna. Hata hivyo usicheleweshe kuvuna ili kuepuka hasara zinazosababishwa na wadudu, wezi na moto vichakani. Uvunaji unapaswa kuanza asubuhi mapema wakati jua limepungua, na kupata usaidizi kutoka kwa watu wengine ili kukamilisha kazi hiyo kwa urahisi.
Pia vuna kwa utaratibu kutoka sehemu moja ya shamba hadi nyingine ili usikose kuvuna baadhi ya mimea, na kisha kukusanya gunzi katika lundo tofauti. Mwisho usirundike mahindi kwenye ardhi wazi ili kuepuka kuharibu gunzi na punje.