Kuweka mahindi kwenye mifuko na kuhifadhi ni shughuli muhimu sana katika mchakato wa kuhifadhi, na unahusisha kupima kiasi au uzito sahihi wa mahindi na kiyafungasha kwa ajili ya kuyauza.
Zaidi ya hayo mahindi yanaweza kupakizwa kwenye magunia ya ukubwa tofauti hii inapaswa kufanywa kwa kupima vizuri na kufungasha kiasi kinachofaa cha mahindi bila kuongeza nyenzo za kigeni kwa ajili ya kuwalaghai wanunuzi.
Tahadhari za uhifadhi
Daima weka vidonge vya kuhifadhia kwenye gunia kabla ya kushona ili kuhifadhi vizuri mahindi kwa muda mrefu. Safisha vizuri chumba kwa kufagia, kupangusa sakafu, na kuziba mashimo ili kuzuia wadudu kuingia. Fyeka misitu iliyokaribu na chumba cha kuhifadhia ili kuzuia kuvutia wadudu. Ziba miunganisho ya paa ili kuzuia ukuaji wa ukungu kwenye nafaka, jambo ambalo hupunguza ubora wa mahindi.
Hata hivyo epuka kutumia mifuko iliyopasuka kuhifadhi mahindi. Pia epuka kumwaga mahindi moja kwa moja kwenye chumba cha kuhifadhia kwani huvutia wadudu. Hifadhi mifuko kwenye mbao zilizopangwa vizuri ili kuepusha ukuaji wa ukungu unaoshusha ubora wa mahindi.