»mafunzo ya uzalishaji wa mahindi»

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=PEciper2XeA

Muda: 

00:17:25
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Ghana E-Agriculture

Mahindi yana aina nyingi na yanaweza kupandwa katika maeneo mbalimbali ya ikolojia ya kilimo. Kila sehemu ya mahindi ina thamani ya kiuchumi.

Mahindi hukua katika aina tofauti za udongo lakini mavuno mengi hupatikana katika udongo wenye kina kirefu, ulio na muundo mzuri, wenye hewa ya kutosha, usio na maji mengi, na tifutifu ambao una wingi wa viumbe hai. Epuka kupanda mahindi kwenye udongo ulio na maji mengi sana, maeneo yenye miti, maeneo yenye kivuli, udongo ulio na mabonge, udongo wenye tope au mfinyanzi.

Kilimo cha mahindi

Daima fanya uchunguzi wa udongo kabla ya kupanda. Kusanya sampuli nzuri kwa kina cha 20cm na upeleke sampuli kwenye taasisi ya utafiti wa udongo kwa uchambuzi. Ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa mahindi inaweza kutayarishwa kwa mikono au mashine kulingana na historia ya ardhi hiyo. Iwapo ardhi ina mteremko, lima kutoka upande moja wa mteremko hadi mwingine ili kuzuia mmomonyoko wa udongo. Mbegu zinapaswa kuthibitishwa na kununuliwa kutoka kwa wauzaji wa pembejeo. Hatua ya kupima uotaji wa mbegu ifanyike kabla ya kupanda. Kupanda kunafanywa kwa kutumia mashine au mikono mwanzoni mwa msimu wa mvua, au wakati mvua inatarajiwa kunyesha kwa aina za mahindi zinazostahimili ukame. Wakati wa kupanda, weka mbolea kwa kina cha 10cm, kisha funika na udongo ili kutengeneza shimo la kina cha sentimita 5 ambamo mbegu hupandwa. 

Weka kilo 250 za NPK siku 10 hadi 14 baada ya kupanda na ongeza juu kilo 125 za salfa ya ammoniamu au kilo 75 za urea kwa hekta.

Udhibiti wa magugu

Udhibiti wa magugu unapaswa kufanywa mapema iwezekanavyo. Hilo hufanywa kwa kubadilisha mazao, kuacha nafasi sahihi kulingana na aina, kupanda kwa wakati, kupalilia na kungoa kwa mikono, kuweka mbolea na kutumia mbegu bora bila magugu. Kemikali pia zinaweza kutumika kudhibiti magugu. 

Wakati wa ukuaji, udhibiti wa magonjwa ya mimea ni muhimu. Ondoa mahindi ambayo yanaonyesha dalili za ugonjwa kwa mfano ugonjwa wa ukungu, uozo wa ma shina.
Mahindi huvunwa kwa mikono yanapofikia ukomavu au kimashine wakati unyevu unashuka chini kati ya 18% hadi 24% . Kisha mahindi hukaushwa hadi chini ya 14% ili kuuzwa au kuhifadhiwa. 
Gunzi la Mahindi yaliyorutubishwa vizuri linaweza kutoa kiasi cha takribani 300g, na punje zilizojaa vizuri. Magunzi makubwa yenye uzito wa hadi 500g yanaonyesha kwamba idadi ya mimea ilikuwa chini sana, na magunzi madogo ni ishara ya rutuba duni.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:55Mahindi yana aina nyingi na yanaweza kupandwa katika maeneo mbalimbali.
01:5602:59Daima fanya uchunguzi wa udongo kabla ya kupanda
03:0004:10Mavuno mengi hupatikana katika udongo wenye kina kirefu, ulio na muundo mzuri, wenye hewa ya kutosha, na mboji.
04:1105:05Ardhi inaweza kutayarishwa kwa mikono au mashine
05:0606:30Tumia mbegu zilizoidhinishwa, na lazima kupima uotaji wa mbegu
06:3107:50Panda mwanzoni mwa msimu wa mvua, au wakati mvua inatarajiwa kunyesha kwa aina za mahindi zinazostahimili ukame.
07:5109:15Ongeza mbolea baada ya kupanda.
09:1612:38Udhibiti wa magugu ufanywe mapema.
12:3913:13Udhibiti wa magonjwa ya mimea ni muhimu.
13:1415:02Mahindi huvunwa kwa mikono yanapokomaa.
15:0317:25Gunzi la Mahindi yaliyorutubishwa vizuri linaweza kutoa kiasi cha takribani 300g.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *