Kuzalisha mimea mipya kutoka kwa shina la mmea mama (Air Layering) | Njia rahisi ya kuzalisha mimea yoyote

0 / 5. 0

Chanzo:

https://youtu.be/BGwzdg0PDHU

Muda: 

00:03:19
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Discover Agriculture.
Hii ni mbinu ya njia ya kuchocheza ukuaji wa mizizi kwenye shina la mmea, na kisha kuukata mara tu mizizi inapokua kwa ajili ya kupandikiza zaidi.
Mbinu hii husababisha sehemu ya juu ya mmea kuunda mizizi ikiwa bado imeshikamana na mmea mama ili iweze kuondolewa na kupandikizwa tena. Ili kutekeleza mchakato huo, unahitaji kisu, mkanda wa nailoni na udongo. Kabla ya kutumia kisu, kisafishe vyema kwa maji ya sabuni ili kuua viini.

Kukata shina

Inchi 0.5–1 chini ya kijicho, fanya mkato wa kina kifupi moja kwa moja kwenye shina ukianzia mbele na kwenda huku ukizunguka shina zima kwa mkato mmoja unaoendelea.
Fanya mkato wa pili wa kina kifupi moja kwa moja kwenye shina ukianzia mbele na kuzunguka shina kwa mkato mmoja unaoendelea. Ondoa gamba kwa uangalifu kwa kukata juu na chini, huku ukihakikisha kuwa haukati ndani zaidi mwa shina.
Kufunga udongo na karatasi ya nailoni
Kata kipande cha karatasi ya plastiki ili kuunda karatasi tambarare ya inchi 12 kwa inchi 18. Chukua kiganja kamili cha udongo wenye unyevu na uufanye kuwa mpira. Fungua mpira na uzungushe shina na udongo ili shina lililokatwa liwe katikati ya mpira. Funga udongo kuzunguka shina hili.
Funga karatasi ya plastiki kuzunguka udongo ili wote ufunikwe kikamilifu kwenye karatasi ya plastiki. Rudisha ndani ya karatasi udongo wowote unaoning‘inia chini na juu ya sehemu iliyofungwa, na kisha ufunge vizuri.

Kumwagilia na kupandikiza

Hakikisha kuwa hakuna udongo unaotoka nje. Rudisha mmea kwenye eneo lake la kawaida la kukulia, na uufuatilie kila wiki. Ingiza maji kwenye udongo kila siku ili udongo usikauke. Inachukua miezi 1–3.
Usitenganishe mmea wakati mzizi wa kwanza unapotokea, lakini mwagilia kwa uangalifu kwani wakati huu mizizi mpya itachukua maji kutoka kwa udongo. Wakati mizizi inaonekana kuzunguka karatasi ya plastiki, mmea huwa tayari kutenganishwa na mmea mama. Ondoa karatasi ya plastiki kutoka kwenye mpira wa mizizi, kata shina chini kidogo ambapo mizizi imetokea na upande mmea popote unapotaka.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:43Mbinu hii husababisha sehemu ya juu ya mmea kuunda mizizi ikiwa bado imeshikamana na mmea mama
00:4401:26Fanya mkato inchi 0.5–1 chini ya kijicho kwa kina kifupi moja kwa moja kwenye shina
01:2702:18Chukua kiganja kamili cha udongo wenye unyevu na uufanye kuwa mpira. Fungua mpira na uzungushe shina na udongo.
02:1902:49Ingiza maji kwenye udongo kila siku ili udongo usikauke
02:5003:19Wakati mizizi inaonekana kuzunguka karatasi ya plastiki, mmea huwa tayari kutenganishwa na mmea mama.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *