Mboga ni chanzo muhimu cha virutubisho na madini. Ubora na wingi wa mboga huamuliwa na mbinu ya uzalishaji.
Wakati wa kurutubisha mboga, hakikisha udongo umetayarishwa vyema na umelimwa kwa kina cha sm 20. Mazao huhitaji virutubisho vya kutosha kwa uwiano unaofaa ili kustawi vyema. Hata hivyo, uwekaji wa virutubisho vinavyohitajika hufanywa kwa kupima udongo.
Uchunguzi wa virutubisho
Chukua sampuli za udongo ili kubaini upungufu wa virutubisho kwenye udongo. Tutumia bomba la kipenyo cha sm 2 na urefu wa sm 15 kupata sampuli 40 za udongo. Changanya sampuli pamoja na uchukue sampuli ndogo za 500g ili zipimwe. Kisha pima pH, na ikiwa iko chini ya 6, ongeza gram 250 ya chokaa kwa mitamraba.
Ili kubaini upungufu wa virutubisho kwenye udongo, tumia kifaa cha kupima udongo, au zingatia dalili za upungufu katika mimea iliyopo.
Umuhimu wa Virutubisho
Mimea huhitaji nitrojeni kwa ukuaji, kwa hiyo viwango vya chini vya nitrojeni hutambulika kwa ukuaji uliodumaa, majani hubadilika rangi, majani yaliyokomaa yanaweza kugeuka manjano na kufa kabla ya kukomaa. Fosforasi huhitajika kwa ukuaji wa mizizi na majani, kwa hivyo upungufu wa fosforasi hutambuliwa na majani kugeuka zambarau. Pia upungufu wa potasiamu hutambuliwa na majani kugeuka njano na kahawia.
Kuweka mbolea
Lima udongo kwa kina cha 10cm, tawanya mbolea sawasawa na uichanganye kwenye udongo. Kwa mimea iliyopandikizwa yenye mizizi ya pembeni, weka mbolea pande zote mbili za mahali ambapo mimea imepandwa. Dumisha afya ya mimea kwa kuongeza NPK na samadi ya mifugo kila baada ya wiki 2–4.
Upe udongo kinachohitajika kwa tija ya juu.