Bamia ni zao linalolimwa sana. Bamia hupenda joto, na hustahimili ukame na kiangazi. Walakini, kumwagilia kidogo na magugu tele husababisha uzalishaji duni wa bamia.
Kukuza bamia.
Panda mbegu bora kupata mavuno bora. Kwenye udongo wa kichanga, mwagilia maji mara tatu kila siku kwa siku 10 za kwanza baada ya kupanda. Majani hunyauka na kukauka hasa katika hali ya jua kali na ukamwe. Kuanzia siku ya kumi hadi siku ya ishirini, mwagilia maji mara mbili tu kwa siku. Baada ya wiki 3, mwagilia maji mara moja tu kwa siku.
Palilia shamba endapo magugu yanazidi bamia, kama wiki 3 baada ya kupanda. Weka udongo kwenye sehemu za chini za shina la mmea ili kuimarisha mizizi yake. Ongeza mbolea oza, samadi au takataka kutoka kwa wafugaji wa kuku. Hii huboresha rutuba ya udongo.