Siagi ya Shea ina virutubisho, hutumiwa kupika, ni vipodozi na chanzo cha mapato. Kufuata hatua za kiusafi pamoja na hatua muhimu za kimfumo husababisha siagi bora kwa watumiaji.
Walakini, epuka usumbufu wakati wa kukoroga kwani kufanya huku hupunguza asilimia ya mafuta. Usitumie vyombo vya chuma kwa sababu vinaongeza sumu kwenye bidhaa.
Kuchambua na kusaga
Osha punje za shea zilizopukuchuliwa mara 2 hadi 3, chambua ili kuondoa punje duni, kausha punje ili zisagwe kwa urahisi. Kisha saga punje ukitumia kinu ili kupata lahamu laini ambayo inapaswa kupozwa ili kurahisisha kukoroga. Lakini hakikisha kwamba unadumisha usafi.
Kupika
Weka lahamu kwenye chombo cha plastiki au alumini kilichopoa, bila kukijaza sana ili kuepuka kumwagika. Ongeza maji ya vuguvugu ili kuwezesha kukoroga kwa urahisi. Wakati wa msimu wa baridi, lahamu huwa baridi kwa hivyo ongeza maji moto na ukoroge kwa muda wa saa 1 ili kutoa dutu nyeupe ya mafuta. Ongeza maji ya vuguvugu ili uchafu uweze kukaa chini, lakini usizidishe maji kwani yanaweza kumwagika. Ondoa dutu nyeupe ya mafuta, ongeza maji na uendelee kufanya hatua hizo kwa mara 2–3. Kisha tengeneza mipira kutoka kwa dutu nyeupe ya mafuta ili kupunguza maji na ladha kali. Onja dutu ya mafuta ili kuhakikisha kuwa haina ladha kali.
Pika dutu yenye mafuta kwa maji hadi kuyeyuka na uchafu uweze kukaa. Acha kupika wakati povu nyeupe itakapoonekana, na mafuta yamegeuka manjano. Poza mafuta na uyamimine kwenye chombo kingine. Kisha ongeza maji safi ili kuwezesha mchakato wa kusafisha. Tenganisha maji na upike tena ili kufanya mafuta kuwa yenye afya na safi.
Poza mafuta, yachuje na kuyaweka kwenye chombo cha plastiki au cha aluminium, kisha ukiweke kwenye chumba na ukifunike. Endelea kukoroga siagi ili kuipa muundo thabiti.