Wakulima huhifadhi mbegu zao kwa msimu ujao, lakini maranyingi mbegu hizo huwa ni za hali ya chini kutokana na madhara ya madudu na magonjwa. Kwa hivyo kuelea mbegu ili kuondoa zilizoharibika huhakikisha kwamba mbegu zako zinatumika.
Kuboresha mbegu ni muhimu ikiwa unataka kuzitumia msimu ujao. Ni muhimu kuanza muzalishaji na mbegu zenye afya. Unajua kwamba mbegu zako zimeshambuliwa, unapofungua chombo kabla ya kupanda na kuona nondo wakitoka ndani na kuruka nje. Pia mashimo madogo ya wadudu yanaonekana. Mbegu zilizoshambuliwa au ambazo hazijakomaa kawaida ni nyepesi kuliko mbegu zenye afya, na kwa hivyo ni rahisi kuziondoa.
Kutenganisha mbegu nzuri kwa mbaya
Safisha mbegu kwa kupepeta. Wakati huu unaweza kuondoa mbegu zozote zilizo na mashimo. Baadaye unaweza kuweka mbegu kwenye maji ili uone ni mbegu gani; ambazo hazijajazwa, vumbi, magada amabayo hayana mbegu ndani, na majani. Sio zote zilizoathiriwa zinaweza kuonekana na kutenganisha kwa kuzitia tu ndani ya maji.
Ili kuondoa mbegu zote mbovu, ni dhahiri kuongeza uzito wa maji. Kwanza, Jaza mtungi safi na maji. Kisha ongeza chumvi na urea halafu uchanganye. Unajua umeongeza chumvi na urea vya kutosha, wakati utakapoona kwamba yai linaelea juu ya maji. Weka mbegu kwenye mchanganyiko na ukoroge kwa mikono. Baada ya muda mchache,utaona mbegu zote mbovu zikielea juu ya maji. Mbegu nzuri zitabaki chini ya mtungi. Ondoa mbegu mbovu yote na uwape kuku wako. Kisha ondoa mbegu nzuri, na lazima zioshwe mara mbili hadi tatu ukitumia maji safi.
Unaweza kuacha maji ya chumvi kwenye chombo tofauti na utumie kunyunyizia miti ya mnazi. Ikiwa maji ni mchanganyiko wa urea, unaweza kuitumia kwa kitalu.