Mbegu za mkunde/ mienze zinazotumiwa kutengeneza viungo zimadimika sana kwa sababu ya ukataji ovyo wa miti mkubwa. Maharagwe ya soya yanaweza kutumiwa kama mbadala wa kutayarisha viungo ambavyo pia hujulikana kama sumbala.
Ili kutengeneza sumbala kutoka kwa maharagwe ya soya, zingatia mchakato kwa makini, na utunze usafi. Kutengeneza sumbala kutoka kwa maharagwe ya soya sio ghali, haichokeshi sana, na ni chanzo cha mapato.
Mchakato
Ili kutengeneza sumbala kutoka kwa maharagwe ya soya, kwanza weka sufuria motoni na ongeza maharagwe ya soya ili kuyakaranga hadi yabadilike rangi. Hii husaidia kupunguza harufu ya soya.
Yakiwa tayari, toa maharagwe kwenye sufuria na uyasage yakiwa moto kwa kutumia mtambo, na uyapepete baadaye. Osha maharagwe mara 2 hadi 3 ili kuondoa chochote kinachoelea.
Chemsha maharagwe yaliyogawanyika, kwenye sufuria. Ongeza chumvi ya potash kwenye sufuria ili kupunguza harufu ya soya, na kuyafanya maharagwe kuwa laini ili yachache. Koroga maharagwe mara kwa mara ili yasiungue. Hakikisha kuna maji ya kutosha kwenye sufuria.
Baada ya maharagwe kuiva vizuri, yaondoe kwenye sufuria na mimina ukitumia kikapu au kitambaa safi ili kuondoa maji. Osha maharage na uyarudishe kwenye sufuria na uyapike tena. Ongeza kiango sawa cha potashi ili kusafisha maharagwe na kuondoa harufu yote.
Wakati sufuria inachemka, toa maharagwe na uyamimine mara ya mwisho. Yaweke kwenye kikapu na mfuko safi, na ufunge kikapu. Hii husaidia kuharakisha mchakato wa kuchacha. Katika msimu wa baridi, funga vizuri mfuko ili kuhifadhi joto ndani. Lakini katika msimu wa joto, maharagwe ya soya yanafaa kuwa yamekauka vizuri ili yasioze.
Weka maharagwe kwa usiku 2 yaweze kuchacha, yabadilishe kuwa lahamu, na kisha kuwa mipira ya ukubwa na umbo unayopendelea.
Weka mipira kwenye wavu na uiweke juu ya moto ili ikauke. Joto husaidia kukausha na kuzuia nzi kuangukia juu mipira ya sumbala.
Sumbala zinapobadilika nyeusi, ziondoe kwenye moto na uzitandaze kwenye mifuko juani. Ili kurahisisha uhifadhi, ponda sumbala ziwe unga.