Maganda ya muhogo ni bidhaa ya muhogo na yanaweza kusindikwa kuwa malisho ya mifugo.
Maganda ya muhogo yanayotumika yasiwe na uchafu kama mizizi mikubwa, na udongo, yaani viondolewe. Tumia maganda mabichi kwa sababu maganda yaliyohifadhiwa huanza kuchachuka, kutoa unyevu na hivyo kuwa magumu kusagwa. Baada ya kuchagua maganda, yakate kate katika vipande vidogo. Saga maganda mara tatu ili kufikia saizi inayohitajika
Kufungasha na kushinikiza
Pakia maganda yaliyokaushwa kwenye mifuko ya plastiki kwa wingi wa kilo 8 hadi 10 kisha ukunje nusu mifuko. Panga mifuko kwenye chuma kwa urefu unaotoa nafasi ya kutosha kwa ajili ya kuweka jeki. Weka vipande vya mbao ili kuhakikisha usambazaji sawa wa shinikizo. Utumiaji wa shinikizo kuondoa maji hadi asilimia 50%. Mifuko iliyoshinikizwa huachwa usiku kucha ili kuchacha na kubadilika kuwa ungaunga wa muhogo. Hii inaweza kulishwa moja kwa moja kwa wanyama au kuhifadhiwa kwa siku 7 kabla ya kuharibika.
Kukausha na kuhifadhi
Ili kutoa ungaunga kavu, endelea kusaga hadi ungaunga uwe laini. Chuja ili kutenganisha ungaunga wa muhogo ulio na ufumwele chache na nguvu nyingi kutoka kwa ule ulio na ufumuele nyingi na nguvu kidogo, na hivyo kutoa bidhaa laini.
Bidhaa iliyosindikwa hukaushwa kwa masaa 6 hadi 8 kwa kuieneza kwenye nyenzo za kukaushia za kawaida. Mara baada ya kukaushwa, bidhaa inapaswa kuwa na unyevu wa kati ya 10% –12%, na inaweza kuhifadhiwa kwa muda wa miezi 4 hadi 6.