»Kusimamisha maharagwe ya kutambaa«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/node/3743

Muda: 

00:15:15
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight

Kujitengenezea vijiti husaidia kuzalisha maharagwe ya kutambaa.

Katika maeneo za nyanda ya juu, maharagwe ya kutambaa huzaa mara tatu kuliko maharagwe ya kichaka. Maharagwe ya kutambaa huhitaji vijiti ili yazae vizuri. Halfu, vigingi/vijiti bora huwa ghali.

Urefu bora wa vigingi/ vijiti

Vigingi vinafaa kuwa na urefu wa mita mbili au mbili unusu. Vikiwa vifupi mno, ncha za maharagwe zitajikunja na kukatika kwa hivyo, mavuno hupunguka. Vigingi vikiwa virefu mno, maharagwe yatajitahidi kutambaa kadri ya urefu huo na kuzaa kidogo. Maharagwe yanapokaribia wiki mbili au tatu, ncha za mimea huaza kutafuta sehemu za kujishikilia na kutambaa.Unafaa kuyawekea maharagwe vigingi wiki mbili baada ya kupanda. Laa sivyo, yatatambaliana kwenye udongo na kuzaa kidogo.

Vigingi vya kujitengenezea

Ili kujitengenezea vigingi, panda miti mbao kama vile mikaratusi au mtukutu. Kata matawi ya miti ili kupata vigingi. Uwezekano wingine ni kutumia vigingi vya nyasi ya napier. Shamba lako halifai kufunikwa na magugu ili maharagwe yasibaki chini yakitambaa juu ya magugu.

Weka vigingi katika mistari kila baada ya nusu mita na uache angalao nusu mita kati ya mistari. Simika vigingi kwa nguvu kwenye udongo ili visiangushwe na upepo mkali. Kila kigingi kinaweza kusimamisha maharagwe matano. Ili kutengeneza henga, weka vigingi vitatu vya urefu wa mita mbili kati ya mistari miwili ya maharagwe, kila kigingi kikiachana kwa mita 5. Unganisha vigingi hivyo katika sehemu ya juu kwa kamba au fito.

Baada ya kuvuna, viweke vingi katika kivuli, ili visipasuliwe na jua. Simamisha vigingi ili pande iliokuwa ardhini iangalie juu, ili maji yatiririke na vikauke kwa urahisi.

Unapovuna mahindi, ondoa magunzi na majani kisha uacha mashina thabiti yakiwa yamesimama ili kuwa vigingi vya maharagwe msimu ujao. Ikiwa mashina ya mahindi si thabiti kutosha, unaweza kuweka vigingi vya miti katika kila mashina manne, na kuvifunga pamoja sehemu ya juu.

Unaweza pia kukuza maharagwe ya kutambaa pamoja na mahindi. Ili kuhakikisha kwamba maharagwe hayathiri mahindi, yapande mwezi mmoja baada ya mahindi.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:42Katika maeneo za nyanda ya juu, maharagwe ya kutambaa huzaa mara tatu kuliko maharagwe ya kichaka
01:4302:45Maharagwe ya kutambaa huhitaji vijiti ili yazae vizuri
02:4604:31Panda miti mbao kama vile mikaratusi au mtukutu
04:3204:42Vigingi vikiwa vifupi mno, ncha za maharagwe zitajikunja na kukatika kwa hivyo, mavuno hupunguka.
04:4304:56Vigingi vikiwa virefu mno, maharagwe yatajitahidi kutambaa kadri ya urefu huo na kuzaa kidogo
04:5705:35Maharagwe yanapokaribia wiki mbili au tatu, ncha za mimea huaza kutafuta sehemu za kujishikilia na kutambaa
05:3605:54Shamba lako linafaa kufunikwa na magugu ili maharagwe yasiweze kukulia kwa ardhi
05:5506:13Weka vigingi katika mistari kila baada ya nusu mita na uache angalao nusu mita kati ya mistari
06:1406:25Kila kigingi kinaweza kusimamisha maharagwe matano
06:2607:58Uwezekano wingine ni kutumia vigingi vya nyasi ya napier
07:5908:23Baada ya kuvuna, viweke vingi katika kivuli.
08:2409:45Simamisha vigingi ili pande iliokuwa ardhini iangalia juu, ili maji yatiririke na vikauke kwa urahisi.
09:4611:32Unapovuna mahindi,ondoa magunzi na majani kisha uacha mashina thabiti yakiwa yamesimama ili kuwa vigingi vya maharagwe msimu ujao
11:3312:20Ikiwa mashina ya mahindi si thabiti kutosha, unaweza kuweka vigingi vya miti katika kila mashina manne, na kuvifunga pamoja sehemu ya juu.
12:2112:53Ili kutengeneza henga, weka vigingi vitatu vya urefu wa mita mbili na umbali wa mita 5
12:5413:30Unganisha vigingi katika sehemu ya juu kwa kamba au fito.
13:3115:15Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *