Afya ya wanyama ni jambo muhimu ambalo huamua ubora na wingi wa bidhaa za ufugaji wa wanyama.
Ufanisi wa chanjo hai ya virusi iliyoreboreshwa hutegemea uwezo wa mnyama wa kuitikia chanjo. Uchanganyaji sahihi, utunzaji na utumiaji sahihi ni muhimu. Pia fanya mashauriano kutoka kwa daktari wa mifugo ili kuzuia magonjwa ya ng’ombe.
Utunzaji wa chanjo
Kwanza, linda chanjo dhidi ya mwanga wa jua, joto, baridi kali na uhifadhi chanjo kulingana na maagizo yaliyoandikwa. Wakati wa kutumia chanjo, weka sindano kwenye jokofu na epuka kumchanja mnyama wakati yupo mnyevu au wakati wa hali ya joto kali.
Vile vile, changanya pamoja chupa 2 zilizopo kwenye kisanduku ili kuamilisha kiambatanisho na katika mchakato huo, tumia sindano safi isio na vijidudu ili kuepuka uchafuzi kutokana na aina tofauti ya chanjo. Ingiza sindano kwenye chupa ya plastiki kupitia kifuniko cha mpira cha chupa. Pindua chupa ya plastiki na ingiza ncha ya sindano kwenye kifuniko cha mpira cha chupa ya glasi. Kipimo kitamwagika kwenye chupa ya glasi kutokana na shinikizo la hewa.
Kisha, ondoa sindano kutoka kwa chupa ya plastiki na utikise chupa kwa upole hadi kipimo kitakapoyeyuka vizuri. Usitikishe chupa kwa nguvu kwani huku kunaweza kuharibu viambatanisho vya chanjo. Ili kuzuia hilo, rejelea kisanduku cha bidhaa kilicho na maelezo ya kipimo na utumiaji.
Tumia mkono mmoja kuinama chupa ya glasi, na mkono mwingine ushikilie bomba la sindano na kuingiza sinadano kwenye kifuniko cha chupa ili kuondoa kipimo cha mchanganyiko wa chanjo kinachohitajika. Kisha, chomoa sindano kwenye chupa na ondoa sehemu fulani ya chanjo huku ncha ya sindano ikielekea juu ili kuondoa hewa ambayo inaweza kuwa hatari kwa wanyama. Funga mnyama na kisha uelekeze sindano mahali sahihi. Kwa sindano ya chini ya ngozi, tafuta mahali sahihi pa kudunga ambapo panapaswa kuwa safi bila uchafu, na tumia sindano mpya iliyosafi. Tengeneza sehemu iliyo kama muundo wa hema kwenye shingo ya mnyama, dunga sindano chini ya hema na hakikisha hautadunga msuli, ingiza chanjo, ondoa sindano, achilia ngozi na uweke alama kwenye mnyama aliyechanjwa.
Baada ya kuchanja, safisha sindano kwa kutumia maji yanayochemka na usitumie dawa za kuua viini. Kwa ufanisi, chanjo hai zote za virusi zinapaswa kutumika ndani ya saa moja baada kuchanganywa, na baadaye tupa sindano kulingana na kanuni.