Kudhibiti kiduma ni muhimu sana kwa kupata mavuno bora.
Mtama na mawele ni mimea iwezao kustahimili hali ngumu ya kiangazi. Lakini gugu chawi/ kiduha huathiri mimea hiyo. Kiduha huvamia mizizi ya mimea na kufyonya maji na virutubisho.
Kiduha/ Dudu chawi
Kiduha ni magugu vimelea. Kiduha lenye maua mekundu hupatikana Afrika mashariki na kusini . Lile lenye mauma ya zambarau limesambaa barani Afrika kwote. Kiduha moja laweza kuzaa laki kadha ya mbegu ndogo.
Kiduha hunawiri kwenye udongo usio na rutuba. Zamani, wakulima walikuwa wakiacha mashamba yao yalioishiwa na rutuba na wakichukua mapya, lakini kwa sasa, hilo haliwezekani tena.
Kusimamia kiduha
Tumia angalao njia tatu tofauti za kuzuia kiduha katika shamba lako. Endelea hivyo mpaka shida ishe. Lakini kuwa muangalifu wakati wote ili kiduha kisirudi. Ukijumuisha na kutumia mbinu tatu au nne za kudhibiti kiduha kwa miaka kadha, basi utaweza kupigana na kiduha kwa haraka.
Suluhisho bora ni kutumia mbolea oza. Hii huboresha udongo kwa kuhifadhi unyevu na kuongeza rutuba.
Unaweza kutumia kiasi kidogo cha mbolea nyeusi ya duka kwa kila tuta. Wakati wa kupiga mtara au tuta, unaweza kutumia mbolea nyeupe. Chaguo hilo ni ghali kwa sababu mbolea hizi hununuliwa bei kali.
Unaweza pia kufanya kilimo msetu cha mbaazi. Panda mstari mmoja wa mbaazi kwa mistari miwili ya mawele na mtama. Hii inaposambaa, itafunika udongo na kuirutubisha, pamoja na kuandamiza kiduha.
Hakikisha unatoa kiduha shambani mwako hata katika msimu wa kiangazi. Laa sivyo, kiduha litatoa mbegu zaidi. Lazima , toa kiduha pamoja na mizizi ili kuepusha mbegu za kiduha kuanguka shambani mwako,
Husisha kijiji chote kuzuia kiduha. Kuungana hupunguza kazi ngumu na huepusha kusambaa kwa kiduha katika mashamba ya majirani.