Ukipanda mpunga kwa kuatika au kupandikiza, waweza kupata mavuno zaidi na udhibiti bora wa magugu. Kwa hivyo usimamizi wa zao lako huwa rahisi.
Ukitawanya mbegu, magugu hutatiza sana. Unapopandikiza au kuatika miche ya mpunga, mavuno yatakuwa bora mara mbili hadi tatu zaidi. Kwa kuongezea unahitaji mbegu chache, kwa hivyo una uwezo wa kuchagua miche za hali ya juu. Mpunga huzaa zaidi, wakati kuna matawi zaidi, kwa sababu kila tawi hutoa wimbi. Kutoa matawi kunategemea na umri wa miche, kina cha kutoa matawi na umbali kati ya mimea.
Jinsi ya kuatika/ kupandikiza
Tumia miche mizuri, lakini hakikisha hujatumia mingi sana kwenye kitalu, kwa sababu utapata miche zilizokonda na dhaifu. Miche zinafaa kuwa na majani manne na kupandikizwa takriban siku 15 hadi 20 baada ya kupanda. Ikiwa miche zina majani matatu tu, hazitaki kina kirefu unapoziatika. Miche zilizo komaa zaidi zina matawi kidogo na zinahitaji muda mrefu kabla ya kuanza kumea.
Sawazisha shamba lako na kukanda udongo ili kurahisisha kuatika miche. Hakikisha kuna kiwango kidogo cha maji shambani siku chache kabla ya kuatika. Ni dhahiri Shamba liwe tayari kabla ya miche ndani ya kitalu hazijakaa wiki mbili. Kabla ya kung‘oa miche unafaa kumwagilia maji ili kupunguza uharibifu kwa mimea. Ziatike haraka uwezekanavyo, ili kuzuia miche kunyauka.
Weka sehemu ya chini ya mche iliyonyeupe kwenye tope, na acha sehemu ya kijani juu ya ardhi. Miche itakua polepole, wakati sehemu ya kijani iko chini ya ardhi. Kukua kwa mimea kutaathiriwa sana iwapo hiyo sehemu ya kijani kibichi itawekwa kwenye udongo. Mizizi ikipandwa kwa kina kirefu, hukosa hewa safi ya oksijeni, hutoa matawi kidogo na itafariki.
Miche za mpunga zinahitaji nafasi ili kunawiri na kutoa matawi. Kwa hivyo unafaa kuongeza miche moja hadi tatu kwa kila kilima cha upanzi. Wakati wimbi linapoanza kuchipuka, matawi huacha kukua na mwavuli huwa unafungwa. Kwa hivyo mpunga huzaa zaidi na una magugu machache.
Pandikiza/ atika mpunga kila baada ya sentimita 20. Wakulima wengine hutumia kamba baada ya kila sentimita 20. Unaweza pia kuweka alama kwa kijiti au kutumia miguu, ama mikono ili kupata vipimo halisi vya kupanda miche. Unafaa kusawazisha vipimo kati ya miche. Ukipanda miche katika mistari itakuwa rahisi kuondoa magugu. Miche zikifariki katika harakati za kuatika, basi zipande upya chini ya muda wa wiki moja.