Kwa kuwa ni zao muhimu na lenye lishe, kilimo cha pilipili na uzalishaji wake hutegemea aina ya teknolojia inayotumika, ambayo huathiri ubora na wingi wa pilipili.
Pilipili hupandwa kwenye vitalu katika mwezi wa Februari na Machi, na hupandikizwa miezi 2 baadaye kwenye udongo unaofaa. Mmea huhitaji mwanga na joto la kutosha, pamoja na unyevu wa 50% –70%.
Kupanda pilipili
Miche hupandwa kwa muachano wa sm 40–50 ndani ya safu, na sm 60–70 kati ya safu. Pilipili hustawi katika udongo tifutifu ulio na mboji. Hata hivyo, muachano wa kawaida ni 1m x 0.5m lakini huu unaweza kupunguzwa hadi mimea 3 kwa kila mita ya mraba.
Vile vile, kumwagilia kunapaswa kufanywa ipaswavyo, na hivyo umwagiliaji kwa njia ya matone ni bora zaidi. Kutengeneza matuta huimarisha mimea na huhimiza ukuaji wa mizizi. Kusimamisha mimea pia kunafanywa ili kuepusha mimea kuanguka.
Kushughulikia pilipili
Wakati wa kupogoa, idadi ya mashina hupunguzwa hadi 2–3, na majani yenye ugonjwa huondolewa. Mwishoni mwa kipindi cha uzazi, ondoa vijicho vyote ili kuhimiza ukomavu, na pia ondoa matunda yoyote ambayo yanatokea chini ya shina la mmea. Hii ni kuhakikisha aina ya matunda ni ya ubora wa juu, na yana umbo bora.
Zaidi ya hayo, mpilipili huhitaji nitrojeni katika hatua za ukuaji za kwanza, wakati fosforasi huwa ni muhimu wakati maua ya kwanza yanapoonekana na katika mchakato wa kukomaa. Potasiamu inahitajika ili kutolea matunda rangi na ubora, wakati magnesiamu huwa ni muhimu katika hatua ya ukomaavu.
Wadudu waharibifu wa pilipili ni pamoja na inzi weupe na chawa, ambayo hudhibitiwa kwa njia ya kibiolojia kwa kutumia wadudu wenye manufaa. Magonjwa makuu ni pamoja na uozo, mnyauko na upele wa bakteria.
Hatimaye, uvunaji hutegemea aina zilizopandwa, na hali ya hewa.