Nyasi ya Napier hupandwa kwa ajili ya chakula cha mifugo ama husindikwa kuwa silaji (lishe lililohifadhiwa)kwa kuongeza molasi, na hivyo lishe hudumu kwa mda mrefu.
Nyasi za napier zilizokomaa zina lishe na madini, na hivyo zinalishwa kwa mifugo.
Baada ya siku 45 nyasi za napier hukua hadi urefu wa futi 3 – 4. Baada ya siku 60 mmea hubadilika hadi futi 5 – 6. Wakati wa kuvuna, kata shina kutoka usawa wa ardhi kwa kutumia mashine ya kukata nyasi ili kuhimiza ukuaji wa shina mpya.
Kupanda hadi kuvuna
Kwanza, lima ardhi ili kulainisha udongo na tengeneza mitaro kwa umbali wa futi 3 ili kuwezesha ukuaji sahihi.
Pili, panda shina kwa umbali wa futi 2 na pembe ya 45, kisha funika na inchi 2 za udongo.
Mwagilia mmea ili kuhimiza uotaji.
Baada ya siku 30 palilia ili kupunguza ushindani wa virutubisho kwa ukuaji sahihi wa mmea.
Kisha weka mbolea ya kikaboni karibu na mashina, na mbolea za maji kwenye majani ili kuhimiza ukuaji wa mimea.
Vuna baada ya siku 60, katakata nyasi na ulishe ndege na ng‘ombe wakati mmea una urefu wa futi 3– 4.
Vuna tena baada ya siku 75 wakati mmea una urefu wa futi 5 – 6 kwa ukuaji wa mashina mapya. Kata kata nyasi na uwalishe wanyama.