»Kupanda mstari kwa mstari«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/node/3288

Muda: 

00:09:10
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight, CBARDP, ICRISAT, KNARDA

Kunde husaidia wakulima kwa njia nyingi. Kunde ni muhimu kwa kupanua mavuno na kupigana dhidi ya kiduha. Ili kujua jinsi ya kupanda kunde kwa usahihi, utajifunza miongozo kadhaa.

Baadhi ya wakulima hupanda kunde aina ya kutambaa (mbaazi) kwa uchache kati ya mtama, mawele na mahindi baada ya zao la nafaka kuimarika. Majani yakidondoka, njia hii ya upanzi huacha udongo wazi mwanzoni mwa msimu na kuwezesha magugu kukua kwa haraka. Kiduha/ gugu chawi amabalo ni mmea lenye maua mekundu na zambarau, ni moja wapo ya aina hizi za magugu. Kiduha hushikilia mizizi ya mazao ya nafaka na hunyonya maji na virutubisho vya mimea.

Faida za Mazao ya kunde

Mbaazi, karanga na soya ni mifano ya kunde. Kunde ni mimea ambayo huzaa maganda, na hutoa chakula, lishe na mapato. Kunde pia huongeza nitrojeni katika udongo na kuboresha rutuba. Udongo ambao umefunikwa vizuri na jamii ya kunde hukaa unyevu na huzuia ukuaji wa kiduha.

Mimea mitego kama vile tumbaku, pamba na ufuta, pia ni jamii ya kunde. Haya yana uwezo wa kuua kiduha. Mimea mitego yana mizizi ambayo hutoa kemikali ambazo huhanda mbegu za kiduha kuota. Lakini kiduha haiwezi kushikilia mizizi ya mimea mtego, na kwa hivyo hufa.

Kufanya mistari

Kunde hukua vibaya ikiwa yamepandwa umbali mkubwa katika uvuli wa nafaka. Ili kupunguza uvuli, panda kwa kutenganisha mistari ya kunde na mazao ya nafaka, kwa hivyo mazao yakuwe vizuri

Ukipanda mistari mitatu ya soya, panda mistari mbili ya mtama katika mwaka ujao. Soya inaweza kuua kiduha, hali kadhali kuleta uwezekano wa kukuza mtama.

Ili kupata mavuno mazuri ya nafaka, unafaa kukuza nafaka kwa hali ya kukaribiana, na kuongeza mbolea oza na mbolea ya madini. Ni rahisi kuweka mbolea ya madini kwenye mazao yalio kwenye mstari.

Kupanda jamii ya kunde ambayo husimama wima, ni rahisi kupalilia kwa jembe au wanyama. Kunde ya kutambaa hufunika udongo na kuua magugu. Kunde hunawiri kwenye udongo wa mbolea oza na inaweza kukua na kufunika udongo vizuri.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:17Baadhi ya wakulima hupanda kunde aina ya kutambaa (mbaazi) kwa uchache kati ya mtama, mawele na mahindi baada ya zao la nafaka kuimarika
01:1802:38Kiduha hushikilia mizizi ya mazao ya nafaka na hunyonya maji na virutubisho.
02:3903:30Kunde ni mimea ambayo huzaa maganda, na hutoa chakula, lishe na mapato.
03:3104:51Mimea mitego yanaweza kuua kiduha.
04:5205:20Kunde hukua vibaya ikiwa yamepandwa umbali mkubwa, katika uvuli wa nafaka
05:2106:10Ukipanda mistari mitatu ya soya, panda mistari mbili ya mtama katika mwaka ufuatao.
06:1107:47Kunde hunawiri kwenye udongo wa mbolea oza na inaweza kukua na kufunika udongo vizuri.
07:4809:10Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *