Kupanda lupine kunaathiriwa na sababu nyingi ambazo ni pamoja na wadudu, magonjwa, usawa duni wa virutubisho vya udongo. Wakulima hukabiliwa na changamoto zinazosababisha ukuzaji duni.
Maharagwe ya lupine yanaweza kupandwa katika nyanda za juu kwa sababu yanastahimili ukame. Yamekithiri madini kama vile protini, fumuele na kalsiamu. Hizi pia huongeza rutuba kwa udongo
Mimea yenye afya
Kamwe usipande lupine kwa miaka 2 katika shamba hilo hilo. Chule (anthracnose) ni ugonjwa hatari sana ambao huathiri lupine tangu wakati wa kuchipuka. Chule hudhuru sana wakati mvua inafuatwa na jua. Chule hutambuliwa na uwepo wa madoa meusi kwenye; majani, maganda na shina ambayo baadaye hukauka. Pia na uwepo wa shina zenye kasoro. Vimelea vya chule huishi katika mbegu na mabaki ya mimea.
Daima weka mbegu mbali na mimea yenye afya. Ugonjwa huo huenezwa kwa mimea mingine kupitia kwa upepo, mvua na watu. Chambua na kubainisha lupine ili kupata mbegu bora. Ondoa mbegu zilizovunjika, zilizo na kasoro, na zilizobadilika rangi. Chambua mbegu kutegemea ukubwa wazo ukitumia wavu au mikono. Tumia mbegu kubwa kwa sababu zina uwezo wa kunawiri na kuzalisha zaidi. Choma mbegu zilizo na ugonjwa ili kuzuia ugonjwa kusambaa.
Suuza mbegu kwa siku kadha ili kuondoa zile zenye ladha kali.