Karanga hukuzwa zaidi magharibi mwa Kenya na hupitia michakato mbalimbali kutoka kwa uvunaji hadi bidhaa za mwisho.
Kuongeza thamani kwa karanga hufanywa kwa kutengeneza siagi ya karanga. Kuelewa misimu ni muhimu kwani karanga ni zao la msimu. Karanga kawaida huanza kukomaa kati ya siku 130–150 kutegemea na aina. Aina maalum ya karanga ni maarufu kwa mashada yake marefu na njugu nyingi, huku aina nyingine ina karanga zilizo kwenye vishada vidogo.
Kuboresha karanga
Hatua ya kwanza ya kuongeza thamani ni kuchuja na kukaanga karanga, ambayo hufanywa kupitia njia maalumu. Njia hii inahusisha kukaanga karanga katika kifaa kinachozunguka kilichopashwa hadi nyuzijoto 426.6°C. Karanga hukaangwa moto hadi 100 ° C kwa dakika 40– 60 ili kuhakikisha zimechomwa sawa.
Baada ya kukaanga, karanga hupozwa hadi joto la kawaida la 25°C na kisha zinaweza kumenywa au kukaangwa jinsi zilivyo.
Kusaga karanga
Karanga husagwa baada ya kupukuchuliwa. Makundi madogo ya karanga huwekwa jwenye mashine, jamba ambalo hutumia muda hasa unapotengeneza siagi nyingi ya karanga.
Hatimaye, baada ya kusaga siagi ya karanga huachwa ipoe kwa saa 36 kabla ya kuwekwa kwenye vyombo safi. Katika viwanda vikubwa siagi ya karanga husukumwa kwenye chombo cha kubadilisha joto kwa ajili ya kupozwa, na kisha hufungashwa.