Bamia hupandwa moja kwa moja kutoka kwa mbegu, lakini kupanda mbegu nyingi katika kila shimo hupunguza ukuaji, na mavuno. Ili kupata miche mizuri ya bamia, tumia mbegu bora na mbinu bora za usimamizi.
Kupata mbegu bora
Unaweza kupata mbegu bora kwa kununua mbegu zilizoboreshwa au mbegu aina za kienyeji. Ili kupata mbegu kutoka kwa aina za kienyeji, tambua mimea yenye mashina kubwa na thabiti, na uvune mbegu za matunda makubwa. Kabla ya matunda yaliyoiva kuanguka, basi fungua matunda na uchague mbegu kubwa, zisizo na uharibifu wala kasoro. Baada ya kuzipata mbegu, zikaushe kivulini kwenye eneo safi la kukaushia, na uzihifadhi katika chombo kisichopenyeza hewa wala unyevu na mwanga wa jua.
Mbinu za shambani
Bamia hukua katika kila aina ya udongo hata bila mbolea, na inaweza kupandwa katika shamba, au vitalu vilivyoinuliwa kwa kuacha nafasi ya umbali na upana wa 40x 80cm. Ili kupata mavuno bora, anzisha shamba lako kwenye jua, na ufanye kilimo cha kwanza ili kufungua na kutifua udongo. Kabla ya kupanda, mbegu zinaweza kuoteshwa, kisha ndio mbegu 2–3 zipandwe kwa kila shimo la kina cha 2cm na kufunikwa na udongo. Ikiwa bamia zimepandwa kwenye vitalu, mwagilia maji baada ya kupanda. Tandaza shamba baada ya mimea kunawiri.