»Kujenga chumba cha Kware«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/quail-housing

Muda: 

00:09:35
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Egerton University

Kufuga kware ni maarufu zaidi kwa wakulima kwa sababu mayai yao yana lishe zaidi, vitamini B1 na B2 na madini kuliko mayai ya kuku.

Kware ni ndege walio kwenye hali ya hatari, kwa hivyo wanahitaji makazi bora. Kizimba kizuri cha kware huhakikisha ulinzi wao.

Faida za ufugaji wa kware

Kware ni rahisi kufuga kwani wanakula kidogo na hawapati magonjwa mara nyingi. Kware hukua haraka na huanza kutaga mayai wakiwa na umri wa wiki 6. Kware ni wadogo kwa ukubwa, na wanaweza kukuzwa katika nafasi ndogo.

Mahitaji

Vifaa vya ujenzi vinaweza kupatikana kutoka duka la vifaa. Kizimba kinachopendekezwa kwa kila ndege 20 kinafaa kuwa na: urefu wa 2 ft, upana wa 2 ft, kina cha 4 ft juu kutoka kwa sakafu. Vifaa ni: 2m bati la chuma, mbao laini (plywood), mbao ya futi 90 iliyo na mita 2 kwa 2. Mbao ya futi 80 iliyo na mita 2 kwa 1, futi 30 za wavu uliyo na 1/2 inchi, misumari na jozi 2 za bawaba zilizo na inchi 3.

Ujenzi wa chumba cha kware

Kware wanahitaji kulindwa kutokana na mvua, na joto. Wanafaa kupata hewa safi. Kware huhitaji chumba cha kuwachunga dhidi ya paka na umbwa kwa sababu wao hutawanyika sana kwa pande zote.

Fremu ya kizimba hujengwa kwa kutumia mbao. Mbao laini (plywood) hukatwa ili kutengeneza sakafu, na kuwezesha kusafisha rahisi, na pia kuzuia kware kutokwama. Kwa pande, nyavu zinabandikwa ili kuhakikisha mzunguko mzuri wa hewa. milango na miguu hujengwa na kuwekwa kwenye kizimba. Makaazi sahihi ya kware huhakikisha ulinzi mzuri unaokusaidia kupata faida kubwa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:30Kufuga kware ni maarufu zaidi kwa wakulima
00:3001:15Mayai ya kware yana lishe zaidi na madini kuliko mayai ya kuku.
01:1502:15Kware ni rahisi kufuga, kwani wanakula kidogo, hawapati magonjwa mara nyingi, hutega mayai mengi, na huhitaji nafasi kidogo
02:1502:30Birds sheltered from rain, sunlight and require fresh air.Kware huhitaji makazi mazuri kuwa wamehifadhiwa dhidi ya mvua, jua, na hupata hewa safi.
02:3002:45Kware huhitaji chumba cha kuwachunga dhidi ya paka na umbwa kwa sababu wao hutawanyika sana.
02:4502:55Toa picha za vizimba ili kupata ruhusa kutoka kwa huduma ya wanyamapori wa Kenya.
02:5504:25Vifaa vya ujenzi vinavyohitajika: mabati ya chuma, mbao laini (plywood), mbao, wavu, misumari na bawaba
04:2505:30Pembe za chumba zinafaa kuimarishwa, mbaolaini hutumiwa kwa sakafu ngumu. Kwa pande, nyavu zinabandikwa.
05:3005:45Safisha sakafu mara mbili kwa siku na pia safisha vyombo
05:4506:15Weka nyavu vizuri ili kuepuka kuumiza kware
06:1507:50Tumia vifaa vinavyopatikana
07:5009:35Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *